Sababu Tano (5) Kwa Nini Biashara Yako Inapoteza Sana Wateja.

Utake au usitake, upo uwezekano mkubwa sana wa biashara yako inapoteza sana wateja. Umeshawahi kujiuliza kwa nini au wewe ndio wale wale umebaki na sababu zile zile kwamba ‘usawa huu ni mgumu, na mambo hayaendi kabisa?’
Ikiwa umekuwa na wewe unatoa sababu kama hizo, nikwambie tu, hapo unajidanganya wewe mwenyewe. Sababu kubwa ya biashara yako kukosa wateja, chanzo kikubwa ni wewe na si mtu mwingine au hali yoyote ile nje na wewe.
Naona unanishangaa kivipi, na mbona mambo yangu yalikuwa mazuri siku za nyuma na kwa biashara hihii, iweje mimi ndio niwe chanzo leo? Nisikilize vizuri, wewe  ni chanzo cha biashara yako kukosa wateja, kivipi, ngoja nikupe sababu;-

 1. Una huduma mbovu kwa wateja wako.
Huwezi kukwepa kukosa wateja kama una huduma mbovu kwa wateja wako. Unaweza usiwe wewe, hapa wanaweza wakawa ni wasaidizi au wafanyakazi wako  ndio wanaokuharibia pasipo wewe kujua kitu chochote na ukaona uko sawa.
Wengi kwa kushindwa kujua kwamba wanahuduma mbovu ndio wanajikuta ni chanzo cha kuanza kupoteza wateja wengi tena bila kujua. Huduma yako mbovu inaweza ikawa kwenye bidhaa au mazingira au  hata jinsi ya kuwahudumia wateja na wakaridhika.
Nini kifanyike?
Hapa kuwa makini sana na mazingira yote yanayoweza kupelekea huduma mbovu ikatolewa, kama wafanyakzi wako, mazingira na bidhaa unazozitoa. Vitu hivyo unatakiwa kuvihakiki mara kwa mara ili visiwe chanzo cha huduma ya hovyo kwako na kupelekea kukosa wateja.
2. Bidhaa zako zimeshindwa kukidhi matakwa ya wateja.
Inapotokea  bidhaa zako zimeshindwa kukidhi matakwa ya wateja wako, hapa unakuwa unawakatisha tamaa wateja wako. Wale wateja wako wanakuwa hawana hamu na wewe na pia hawana hamu hata na biashara yako, hivyo ‘automatic’ unakosa wateja.
Hakuna mteja ambae atakuwa na furaha ya kununua bidhaa zako ambazo hazijaweza kumsaidia. Mteja hyu ni lazima ataachana na wewe na kwenda kutafuta huduma ambayo inamsaidia hata iwe kwa gharama kubwa, ataifata tu popote.
Nini kifanyake?
Unatakiwa kutengeneza au kutoa bidhaa bora sasa. Ili hili lifanikiwe unatakiwa kufanya kazi na watu ambao ni wataalamu kwa hilo. Pia si hivyo tu jaribu bidhaa zako hizo kabla haijawafikia wateja wako na kujiridhisha je, zinafaa au hazifai?
3. Hauonyeshi thamani kwa wateja kikamilifu.
Kinachowafanya wateja wanunue huduma au bidhaa zako ni thamani wanayopewa na wewe. Pia kitu kingine kinawachowafanya wateja wanunue ni kwa sababu unauza kwa bei ndogo bali ni ile thamani kubwa wanayopewa, hivi ni vitu vya msingi sana.
Kama utajua jinsi ya kutoa thamani sahihi na inayoendana sawa sawa na mteja wako utafanikiwa, kama ni suala la bei mbona kila mtu anaweza kupunguza bei, ila si kila mtu anaweza kutoa thamani sahihi itakayombakisha mteja kwa miaka mingi.
Nini cha kufanya?
Hakikisha unatoa thamani iliyo kamili kwa wateja wako. Wewe pamoja na ‘timu’ yako unatakiwa kufanya kazi sana ili kuweza kuwalinda wateja kwa kuwapa thamani sahihi. Ukumbuke thamani kwenye biashara ndio chanzo cha mafanikio makubwa.
4. Biashara yako ina mwendelezo mbovu.
Katika biashara na katika maisha kwa ujumla, kufanya kitu kwa mwendelezo/consistent pasipo kusimama na kwa muda mrefu, kunaleta kuaminiwa sana. Huwezi kufanikiwa katika biashara kama leo hii umeifungua na kesho umeifunga au unafanya unavyotaka kisa ni biashara yako.
Watu wanaodumu katika biashara na wanaofanikiwa katika maisha, ni watu ambao wanafanya vitu  vyao kwa mwendelezo na kwa muda mrefu. Utakuta mtu anafanya jambo la aina fulani kwa muda mrefu, lakini mafanikio anakuja kuyaona baadae.
Nini kifanyike?
Jenga nidhamu au utaratibu wa kufanya biashara yako kwa mwendelezo sahihi, pasipo kujali kuna wakati unakutana na changamoto au la. Wewe kazana kuweka juhudi kila siku kwa kufanya kitu kilekile hata kama hakitakupa matokeo leo makubwa lakini kifanye.
5. Mbinu zako za kimauzo zimepitwa na wakati.
Inapotokea mbinu zako za kimauzo zimepitwa na wakati huwezi kuendelea kuwapata wateja wengi. Hapa ndipo maana kampuni kubwa zikaja na kitengo cha huduma kwa wateja ili kila siku kuweza kumudu kuboresha huduma ili kuleta mafanikio.
Kama kila wakati utaendelea kuwa na mbinu zile zile za kimauzo pasipo kuzibadilisha na kutegemea muujiza utakaokupa wateja wengi, naomba nikwambie kwenye hilo jambo lisahau kabisa. Ni muhimu ukabadilika kwanza wewe na wasaidizi wako.
Nini kifanyike?
Kila mara pata mafunzo ya jinsi ya kuboresha huduma kwa wateja na unaweza kuyapata kupitia semina au warsha mbalimbali za kibiashara.  Pia jenga urafiki na wateja ili wakusaidie kupata wateja wengine zaidi na zaidi ili kufikia mafanikio.
Kwa kumalizia niseme hivi, unapoona biashara yako inakosa wateja, ukumbuke huo sio uchawi au bahati mbaya. Unatakiwa kutambua kwa uwazi kabisa kwamba zipo sababu kama hizo na wengi wanakuwa hawazijui.
Ninaamini kwa kuzijua sababu hizo leo, basi utazifanyia kazi na kuamka kwenda kuisimamisha biashara yako kwa kishindo kikubwa.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,







Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel