Acha Kuishia Hapa Tu, Fanya Mabadiliko Ya Kudumu Ya Maisha Yako.

Leo ni siku ambayo watu wengi wanaamini wakati wa kufanya mabadiliko mapya umewadia. Kwani nini wanaamini iko hivyo ni kwa sabbau leo ni mwaka mpya, kwa hiyo imani ile ya kubadilisha mambo leo iko juu sana.
Kama unaamini hivyo kwamba kuna sehemu ulishindwa na huu ndio wakati wa kufanya mabadiliko kwako, tafadhari, fanya mabadiliko hayo na acha hata kidogo kuishia kati, kama ni mabadiliko hayo endelea kuyafanya maishani mwako kote na yasiwe ya kitambo.
Mabadiliko ya kweli katika maisha yako hayaji tu kwa sababu leo ni mwaka mpya, bali yanakuja kwa sababu unatakiwa kubadlili maisha yako haswaa na kila siku pasipo kusubiri kitu chochote cha nje ikiwa pamoja na msukumo wa nje.
Leo hii kama wewe mwenyewe umeamua kweli iwe siku yako ya mabadiliko, naomba uzaliwe upya kweli. Acha kuishia tu kusheherekea mwaka mpya na kusahau kufanya mabadiliko ya kweli na ya kudumu katika maisha yako.

Usiwe mtu ambae umejipa ‘ubatizo’ wa kuzaliwa upya na halafu kesho nikukute unarudia maisha yale yale ya zamani yanayokurudisha nyuma. Weka mikakati mizito ya kuamua kubadilisha maisha yako kweli na acha lelemama.
Kama umeamua kufanya mabadiliko ya kweli fanya kweli, acha utoto na acha kujirudisha nyuma kwa namna yoyote ile ambayo ni hatari kwa afya ya mafanikio yako. Jambo la kuzingatia sana kwako ni kuhakikisha lazima unasonga mbele .
Najau kwa miaka mingi umepitia makubwa ya kupanda na kushuka, lakini hiyo nikwambie tu inatosha, sasa ni wakati wako wa kuleta mabadiliko ya kudumu katika maisha yako na mabadiliko hayo unaweza ukayaanza leo.
Asikuzuie mtu, kisikuzuie kitu, amua kufanya mabadiko ya kweli katika maisha yako na mabadiliko hayo yasiishie tu katika siku za mwanzo za mwaka bali yawe endelevu kizazi na kizazi hadi iwe kumbukumbu kwako kubwa na kudumu.
Ngoja leo nikupe baraka zote za kukutakia heri ya mwaka mpya, lakini mwaka huu uwe kweli wa mabadiko ya kudumu kwako na usiwe mwako ambao uwe wa majuto kwako tena kama ambavyo imekuwa pengine ikitokea.
Naamini hilo litafanikiwa kwako na Mungu atakubariki ikiwa utachukua hatua sahihi. Kama nilivyosema, acha kuishia kusheherekea mwaka mpya tu, bali amua kufanya mabadiliko ya kweli ya maisha yako.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,








Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel