Jifunze Unavyoweza Kupanda Moyoni Yale Unayotaka Yatokee Katika Maisha Yako.
Thursday, May 19, 2022
Ipo namna ambayo unaweza ukapanda au ukatengeneza yale unayotaka na yakatokea maishani mwako. Hiki si kitu cha kushangaza tena uwezo huo wa kuumba maisha yoyote yale na uyatakayo unayo na ni jambo linalowezekana kabisa.
Kwa mfano, kama unataka usalama jishawishi moyoni mwako kwamba uko salama, kama unahitaji pesa jiambie nina pesa nyingi. Kama unataka chochote kile ukitakacho, ni zoezi tu la kukazana kujiambia kwamba unataka kitu hicho ukitakacho..
Chochote unachohitaji anza kujiambia kwamba unacho tayari. Kitu cha msingi kwako ni wewe kubadilika kuingia katika masafa unayohitaji hata kabla ya mazingira kubadilika ndipo nazingira yatafuata ya kukipata kitu hicho.
Hata kidogo usiseme sitaki magonjwa, sitaki kuumwa umwa, sitaki mwanamke mwemba mba, sitaki mwanamume maskini, maana hivyo unavyovikataa ndivyo utakavyoletewa. Unajua kwa nini hivyo ndivyo utakavyoletewa, sikiliza.
Mawazo ya kina yanafanyia kazi yanachopelekewa,na hayana upembuzi wowote, hayana akili kama wewe kujua kwamba hili linakataliwa au linakubaliwa. Mawazo haya yanajua kile tu unachokisema ndicho unachokitaka na yanakupa kweli.
Ndio sababu wengi sana wameletewa vile vitu walivyokuwa wakivikataa sana. Kama hauhitaji umaskini basi usiuwazie umaskini bali wazia utajiri. Jiambie mimi ni tajiri, huku ukijionesha wewe ni aina gani na kiwango gani wewe ni tajiri, jiambie wewe una pesa nyingi.
Kile mlichokuwa mnakosea ni kule kumueleza Mungu matatizo yako, mimi nateseka,mimi naonewa baba, mimi ni mgonjwa, baba mimi sina pesa. Yale mliyokuwa mkimtajia Mungu ndiyo mliyokuwa mkirudishiwa zaidi.
Akili za kina ndizo zilizokuwa zikitendea kazi mazungumzo yenu hayo na kusema ukweli hizo hazina akili ya kupambanua bali zina akili ya kuumba kinachohitajiwa. Unaona sasa kila unachokitajja ndicho kinachotokea kwenye maisha yako.
Mawazo ya kina yana nguvu mara 90 ya mawazo ya kawaida, na linapofanikiwa jambo kuumbika humos basi hufanyika mara moja, ni nguvu ya uumbaji. Kwa lugha rahisi mawazo haya ya kina ndio ynayoumba maisha yako hata kama wewe hujui.
Jambo la msingi kwako usipeleke humos vitu usivyohitaji, peleka humos vitu unavyohitaji vitokee maana kila kitakachofanikiwa kuumbika humos hutokea. Kwa sababu hii dio maana unatakiwa uwe makini sana na kile unachokiongea maana unakiumba.
Ni sababu mojawapo kwa sababu hatuna zuri na baya kwa sababu kwa kadiri unavyosema lile ndilo baya unalipa uwezo wa kufanyika tena na tena kwa sababu chochote unachokandamiza unakivuta zaidi, kukandamiza ni kukikataa na hivyo kukilazimisha kiingie ndani ya mawazo ya kina, ni sawa na kukandamiza bomu.
MAKALA HII IMEANDIKWA NA NDUGU, JOSEPH JACKSON WA MWANZA TANZANIA, MAWASILIANO 0754 688 219.