Mambo Matatu Ya Kukusaidia Kukuongoza Kwenye Safari Ya Ujasiriamali Na Kukupa Mafanikio Makubwa.
Sunday, May 15, 2022
Kila mtu anatamani biashara anayoifanya ifanikiwe, kila mtu anatamani akiingia kwenye ujasiriamali mambo yake yanyooke sana na yawe ya mafanikio makubwa. Hiki ndicho kitu ambacho watu wengi sana wanapenda kiwe kwenye maisha yao.
Hata hivyo uelewe hivi, unapochagua kuingia kwenye biashara, ujue kabisa umechagua kabisa kuingia kwenye ulimwengu wa wapambanaji haswa, yaani ulimwengu wa ujasiriamali. Hivyo, unapoingia kwenye dunia ya ujasiriamali kuna mambo lazima uyajue kwanza.
Pasipo kuyajua mambo haya, nakuhahakikishia kabisa, utakwama sana na itafika mahali utajiona wewe si kitu na si lolote. Pengine jiulize, mambo hayo ni mambo gani ambayo yatakusaidia kukuongoza kwenye safari ya ujasiriamali na kukupa mafanikio?
1. Tambua jinsi ya kukabiliana na hali yoyote ile.
Unapoinguia kwenye biashatra na huku ukaingia na mawazo ya aina moja tu kwamba mimi naenda kupata, basi utakuwa unajiweka kwenye wakati mgumu sana. Kwa kuwa umechagua kuingia kwenye biashara ujie kabisa kuna kupata na kukosa.
Inapotokea umepata unashukuru Mungu, lakini inapotokea umekosa pia unashukuru Mungu kwa matokeo hayo na kuchukua uamuzi wa kusonga mbele. Usiingie kwa akili ya kupata moja kwa moja utapotea.
2. Tambua kuna hali hatarishi.
Zipo hali hatarishi nyingi sana au ‘risk’ hasa pale unapochagua kuingia kwenye ulimwengu wa biashara. Hali hizi hatarishi unatakiuwa kupambana na kukabiliana pasipo na hofu yoyote kwani kwa kuzishinda huko ndiko unafanikiwa.
Kama umeamua kuingia kwenye biashara au ujasiriamali na ukawa mwoga na hali hiz hatarishi basi utakuwa unapotea. Kwa kujua kuna hali hatarishi basi itakuwa ni njia sahihi ya namna ya wewe kuongozwa kwentye njia ya mafanikio ya ujasiriamali wako.
3. Tambua kukabiliana na hofu.
Wale wanaofanikiwa si kwamba ni watu ambao hawana hofu kabisa, ni watu ambao wana hofui kama wewe ila wanaamua kukabiliana na hofu zao hivyo hivyo pasipo kujali nini kinaendelea ndani mwao juu ya hofu hizo.
Hata wewe unaweza kukabiliana na hofu hizo hivyo hivyo kila siku. Kuna wakati utakutana na mambo yatakayokuwa magumu kwako lakini unatakiwa kujifunza jinsi ya kukabaliana nayo na uatafika wakati utakuwa mshindi kweli.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com