Kama Unataka Kuwa Tajiri, Anza Kufanya Biashara Hizi Kwanza.
Monday, May 23, 2022
Katika dunia ya sasa zipo biashara nyingi ambazo mtu anaweza akachagua mojawapo na kuifanya, na kwa kuchagua huko biashara hiyo inaweza ikampa mtu huyo mafanikio makubwa na hadi kuweza kufikia utajiri mkubwa.
Hata hivyo pamoja na wingi huo wa biashara, kwa mujibu wa tafiti ambazo zimefanywa hivi karibuni zinaonyesha zipo biashara ambazo ukizifanya zinaweza zikakufanya ukawa tajiri kwa haraka sana au zikakurahisishia njia ya wewe kwenda kwenye ubilionea wako.
Biashara hizi si mpya sana masikioni mwako unazijua, hapa nakukumbusha ili uweze kuzingatia kwa jicho la tofauti na pia kuzifanya kwa namna ya tofauti. Kwa kufanya biashara hizo kwa utofauti, utakuwa umemudu kuweza kupiga hatua ya kufikia mafanikio yako.
Biashara hizo ni zipi? Zifuatazo ni aina za biashara ambazo ukizifanya zitakupa mafanikio makubwa na yenye tija kwenye maisha yako.
1. Usafiri.
Moja ya biashara ambayo inaaminika hasa kwa bara la afrika ikiwa utaifanya kwa utulivu na ukafata misingi yake ni biashara ya usafiri. Hapa unaweza ukawa na kampuni yako ya kusafirishia abiria kutoka sehemu moja na kwenda nyingine.
Kwa sasa hitaji la usafiri bado ni kubwa, kama si mjini hata kijijini. Watu wanataka kusafiri kila siku na kwa bahati mbaya wengi hawana uwezo huo wa kumiliki vyombo vya usafiri. Hii ni mojawapo ya biashara ya kuifikiria kuifanya kama unaweza, kwani itakupa mafanikio sana.
2. Afya.
Kama pia utajikita na kufanya biashara inayohususha mambo ya afya, basi upo uwezekano mkubwa zaidi wa wewe kufanikiwa sana. Huduma za afya katika maeneo mengi bado hazijafikiwa kisawasawa na zinahitajika kweli.
Hivyo kwa kufanya biashara hii, kama ukifungua hospitali au zahati au duka la dawa, utapata pesa na hapo pia utakuwa imeisaidia jamii. Kikubwa kubali kuzunguka kuangalia ni wapi ambapo ukifanya huduma au biashara hii wewe itakulipa.
3. Chakula.
Hakuna mtu asiyekula, hiyo ikiwa na maana ukianzisha biashara ya vyakula na ukaifanya kwa ufanisi mkubwa utafanikiwa. Hapa unaweza ukauza chakula, lakini si maanishi uje na picha ile ya mama ntilie ‘pasee.’
Ukiamua kuja na biashara ya kuuza chakula ifanye kwa ukisasa zaidi. Zipo sehemu bado nyingi zinazohitaji huduma hii ya chakula safi, mazingira safi, lakini hawaipati kwa uhakika kwahiyo unatakiwa ujue jinsi ya kuanza ili uanze kupiga pesa.
4. Viwanda vidogo vidogo.
Huwezi kuendelelea sana kama utaendelea kuwa mlanguzi wa biashara za watu wengine. Changamsha akili na anza mchakato wa kuweka viwanda vidogo vidogo ambavyo vitasaidia wewe kuweza kukupa kipato kikubwa.
Uzuri wakuwa na kiwanda kidogo wewe ndio unakuwa mzalishaji wa kwanza kwa hiyo ni lazima utapata faida kubwa sana. Hapa unaweza ukatengeneza kiwanda chako cha kutengeneza juisi au unga wa sembe na lishe, uamuzi ni wako.
Kwa kuhitimisha, hizi ni baadhi ya biashara chache tu, ambazo unaweza ukazifanya na zikakupa mafanikio makubwa. Uamuzi ni wako uanze na biashara ipi.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com