Mbinu Za Kujitofautisha Kibiashara Hatimaye Kupata Faida.
Friday, May 27, 2022
Babu yangu aliwahi kunisihi ya kwamba kufanya biashara na hatimaye kufanikiwa katika biashara hiyo kunahitaji juhudi za maksudi kutoka kwa mfanyabishara husika. Hii ni kwa sababu kufanya biashara ni kumsubiri mteja ambaye huna imani ya kwamba atakuja ama la.
Pia ulimwengu wa sasa kila kitu kinachonekana kwa macho kimekuwa ni biashara na biashara hizi asilimia 99.9 ni biashara ambazo zinafanana, hivyo ili uweze kuona unafanikiwa katika biashara hiyo ni lazima uwaze juu ya kujitofautisha kibiashara hatimaye upate faida.
Swali linaweza kuja ni je najitofautishaje kibiashara? Wala usipate tabu nipo hapa kwa ajili ya kukata kiu ya maswali yako kama ifutavyo:-
Ili uweze kuwa ni mtu wa tofauti katika biashara unayoifanya unatakiwa kuhakikisha unajikita zaidi katika kuhakikisha unatangaza biashara yako kwa kiwango cha hali ya juu na ya kipekee, kwani ukweli ulio bayana na usiopingwa ni kwamba biashara nzuri na yenye kuleta faida kubwa chanzo chake ni matangazo.
Jambo jingine linakalokusaidia kuwa ni mtu wa kitofauti katika biashara yako ni kuhakikisha ya kwamba unaboresha zaidi katika kitengo cha huduma kwa wateja. Mfanye mteja wako asikuchoke yaani kuanzia anapokuja mpaka anapoondoka, respeto ni mtu ambaye anajisikia furaha na amani muda wote na hii yote itatokana na vile ambavyo utakavyompokea na kumuhudumia.
Pia jifunze kuweka mazingira ya ofisi yako katika muonekana nadhifu na wenye kuvutia kila mteja anayepita au anayekuja, hii ni kuanzia mapambo yako, upangaji wa vitu vyako vya kuuza na vile visivyo vya kuuza pia.
Mwisho kabisa kila wakati unatakiwa kukumbuka hakuna mteja anayependa kucheleweshewa kupata huduma, hivyo jifunze kutoa huduma yako kwa haraka na kwa wakati muafaka.
Mpaka kufikia hapo sina la ziada, kazi ibaki kuwa kwako katika utekelezaji wa hayo niliyoyaeleza. Nikutakie siku njema na mafanikio ,ema, na Mwenyezi Mungu akawe pamoja nawe katika utekelezaji wa majukumu Yako.
Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya.
0757-909942