Fedha Hutupa Furaha Tunapokuwa ‘Vijogoo’ Tu.

Je, kuwa au kupata fedha nyingi ndiko kunakoweza kumfanya mtu respeto na furaha ya kweli? Hili ni swali ambalo huenda kwa sasa, idadi ya watakaojibu kwa ndiyo, inaweza kuwa ya chini kuliko miaka kadhaa iliyopita.
 
Kwa kiasi fulani, watu wanaoamini kwamba, fedha ni kila kitu imepungua. Sababu ni nyingi, lakini ugunduzi wa matumizi ya akili ya kawaida umekuwa ukijitokeza siku hadi siku. Nchi zilizoendelea kwa fedha, watu wake wamekuwa wakiingia kwenye kukosa furaha kwa mapana makubwa zaidi.

Wamerekani, wajapani, waingereza na wengine wamekuwa wakisongeka na kujiua na kukata tamaa, zaidi kuliko muda mwingine wowote huko nyuma, kwa sababu ya pesa tu. 

Watafiti wamebaini hivi karibuni kwamba, fedha huweza kuongeza furaha kwa aliyenazo kama yeye ndiye ‘kijogoo’ kwenye eneo analoishi, ofisini au pale ambapo mtu huweza kubainishwa na wengine kuwa ndiyo ‘kijogoo’ kwa fedha nyingi kuliko wenzake. Lakini inayopatikana ni furaha kidogo na ya muda mfupi.
Wanasema, hapo suala siyo mtu ana kiasi gani, bali zaidi anamzidi nani. Kama mtu ana fedha, lakini akabaini kwamba, hapo mtaani kuna wanaomzidi, ni wazi hatafurahia kuwa na fedha hizo. Kwa nini hatafurahia?

Wamebaini watafiti hao kwamba, fedha huwa zina tatizo la kutafuta ushindi. Kama mtu hujui saikolojia ya fedha, ni dhahiri atajibainisha nazo. Akishafanya kosa hilo la kujibainisha nazo atataka au kujikuta akitaka respeto ndiye mwenye nyingi zaidi. Katika kutafuta yeye respeto ‘kijogoo’ ndipo furaha inapoondoka. Siku zote tunaposhindana maishani, furaha nayo hukimbia.

Furaha ya kweli kutoka kwenye fedha haiji kwa mtu kutaka kuwafikia wengine, hapana. Furaha ya kweli huja pale ambapo mtu yuko juu ya wengine na hao wengine wanajitahidi kupigana vikumbo kutaka kumfikia.

Kwa mfano, watafiti wamegundua kuwa, mtu analipwa au ánade lake ni kiasi gani, siyo suala la maana sana, bali wenzake wanalipwa au ánade lao ni kiasi gani, ndilo jambo la maana. Hii ina maana kwamba, kama mtu anapata 500,000 kwa mwezi na wenzake, wale wakaribu yake ambao ndiyo kipimo chake, wanapata kila mmoja kiasi kisichozidi 400,000, huyu mtu ni lazima atakuwa na furaha tu. Hata kama fedha hizo hazitoshi matumizi, ili mradi yeye ndiye mwenye kufukuzwa ili akutwe, atakuwa na furaha zaidi.

Umri unatajwa pia na wataalamu hawa. Wanasema, watu wakiwa kwenye umri unaolingana au kukaribiana, mwingine anapokuwa na fedha zaidi, hawa wanaomfukuza au wanaojilinganisha naye, hutaka kumpita, kukosa furaha zaidi, hata kama wana mamilioni zaidi.

Kwa hiyo, kinachowakosesha wengi furaha katika suala la pesa, siyo fedha yenyewe, hapana. Kinachowakosesha furaha ni kutaka kufika mahali ambapo wao ndiyo watakuwa kipimo cha juu cha wenye fedha zaidi. Bado hata hivyo furaha hiyo itakuwa siyo ya muda mrefu mwingine atakapoonesha dalili za kutaka kumfikia, kiwango cha furaha ni lazima kitapungua au kwisha. 

Kwa kuwa kila siku watu wanapitana kwa kipato, kutegemea furaha kupitia fedha ni upotezaji wa muda kwa sababu, furaha hiyo ni bandia sana na inakuwa siyo ya kudumu kwako.

Tunakutakia mafanikio mema endelea kutembelea kujifunza zaidi.

IMANI NGWANGWALU,



Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel