Thamani Ya Mafanikio Kidogo Ya Leo, Ni Utajiri Tosha Kwako Kesho.

Ni rahisi tu unaweza kupuuza mafanikio uliyoyapata leo kwa kuona mafanikio hayo ni kidogo sana na hayakusaidii kwa chochote. Hali hiyo inatokea kwa wengi na kutokana na hali hiyo watu hao hujikuta wakizidi kuporomoka sana kimafanikio.
Mathalani, tuchukulie umefanya biashara ya aina fulani na ukapata faida kidogo tu,ambayo kwa mtazamo wako, unaona faida hiyo ni kidogo, hivyo unaamua kuitumia yote kwa kudharau kwamba faida hiyo ni kidogo sana na haina msaada.
Kama ikatokea ukafanya hivyo katika mazingira yoyote yanayofanana na kama nilivyoeleza hilo ni kosa kubwa kimafanikio. Iko hivyo kwa sababu mafanikio yako yanategemea sana  leo yako unafanya nini cha faida hata kama ni kidogo kama nukta. 
Umuhimu wa mafanikio ya leo hauwezi kupuuzwa kwa sababu eti mafanikio hayo uliyo yapata kidogo. Unatakiwa kuchukulia kila aina ya mafanikio hata kama ni madogo sana kwa uzito ule ule mkubwa.
Hakuna anayeamka asubuhi akiwa amefanikiwa. Mafanikio yote duniani yanajengwa kidogo kidogo tena kwa muda mrefu. Hivyo unapofanikisha jambo fulani hata kama ni dogo usilidharau, linathamini kwani litakupa mafanikio makubwa baadae.
Kitu usichokijua pengine, thamani ya mafanikio yako ya leo hata kama ni kidogo, ni msingi mkubwa wa utajiri wako wa kesho. Ili mafanikio hayo madogo yakusaidie na usiyapuuze, anza kuyafanyia kazi hivi;-

Ni rahisi tu unaweza kupuuza mafanikio uliyoyapata leo kwa kuona mafanikio hayo ni kidogo  Thamani Ya Mafanikio Kidogo Ya Leo, Ni Utajiri Tosha Kwako Kesho.
Thamani mafanikio yako hata kama ni kidogo.
Mosi, weka malengo ya muda mrefu ya kimafanikio.
Katika kuweka malengo ya muda mrefu ya kimafanikio usijali kitu chochote, hata kama leo hii upo kwenye changamoto kubwa sana na unapata mafanikio kidogo, wewe malengo hayo jiwekee na anza kuyafatilia siku hadi siku na ipo siku utashangaa unayafanikisha.
Jiulize malengo uliyonayo ni yapi? Je, una malengo ya kujenga ‘Logde’ au una malengo ya kujenga hoteli kubwa? Bila kujitilia shaka yaandike malengo hayo na ikiwezekana chora picha ya hicho unachokitaka ili ukumbuke vizuri.
Kwa jinsi ambavyo malengo yako yatakuwa karibu na wewe yaani hapa namaanisha kwenye picha na kwenye maandishi, ndivyo utajikuta unazidi kuchukua hatua za kufikia malengo hayo hata kama ni kwa kidogo kidogo.
Sasa ni nini kinachoshindikana, naamini hakuna, kama iko hivyo weka malengo yako. Usiue ndoto zako eti kisa upo kwenye wakati mgumu wa kimafanikio au kile unachokipata ni kidogo. Weka malengo yako unayotaka kuyafikia hata kama mfukoni mwako hauna kitu.
Pili, Tatua matatizo yako ya leo, kabla kesho haijafika.
Ukijifunza kutatua changamoto zako mapema kila siku, hiyo itakusaidia sana kuweza kupiga hatua na kuondoa kuahirisha ambako inaweza ikawa chanzo cha kukwamisha. Kitu unachotakiwa kukitatua leo, kitatue bila shida.
Kwa nini nakwambia hapa utatue changamoto zako mapema? ni kwa sababu changamoto zinapokuwa ndogo zinakuwa hazihitaji gharama kubwa sana na hilo litakusaidia kwa sababu ya kile kidogo unachokipata.
Ni rahisi kujiingiza kwenye matatizo ya kila siku, ikiwa kila kitu hutakitatua kwa wakati. Unatakiwa kutatua kila changamoto mapema sana ili uweze kuishikwa uhuru na mafanikio kwa kile kidogo unachokipata.
Kwa hiyo mpaka hapo unaona mafanikio yoyote unayopata hata kama ni madogo, yanaweza kukusaidia kufanikiwa na ukafika mbali ikiwa utayafanyia kazi vizuri na kwa umakini mkubwa. Chukua hatua.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel