Mambo Matano (5) Muhimu Yatakayokusaidia Kufikia Kilele Cha Mafanikio Yako
Sunday, June 19, 2022
Siri kubwa iliyopo katika kuyafikia mafanikio yako ipo katika kuzifahamu mbinu zitakazokusaidia kuweza kuyafikia mafanikio hayo. Wengi tumebweteka kimwili na kiakili huku tukizani labda mafanikio chanzo chake huwa ni bahati nasibu, uchawi na mengineyo mengi yasiyokuwa na ukweli wowote ndani yake.
Hata hivyo ukweli ni kwamba yapo mambo muhimu ambayo yatakusaidia kuweza kufikia kilele cha mafanikio, na mambo hayo ni:
1. Chukua hatua kila siku.
Mafanikio ni mchakato usiokuwa na mwisho, hivyo basi kwa kila kitu ambacho unadhani kinakupa mwanga wa kuelekea kwenye kutimiza malengo yako ni vyema ukachukua hatua za utekelezaji wa jambo hilo.
Watu wengi sana ni wazuri sana wa kuwaza mambo mengi sana ya msingi ila linapokuja sula la kuchukua hatua wamekuwa ni watu wavivu sana wakuweza kufanya hivyo na matokeo yake watu hayo wamekuwa wakijitengenenezea ukata wao wenyewe. Hivyo kila wakati jifunze kuchua hatua sahihi kwa kile unachokifanya au unachotaka kufanya.
2. Jifunze kuweka viupambele.
Kazi yeyote inayofanywwa isiyokuwa na vipaumbele ni uchafua, kama ulivyo uchafu mwingine, unashangaa wala usishangae huo ndio ukweli.
Watu wengi wanashindwa kutuliza kiu ya umaskini hii ni kwa sababu watu hao wameshindwa kutambua ni kwa namna gani wanaweza kupanga viupembele kwa vile vitu wanavovifanya.
Kupanga vipaumbele humsaidia mtu husukia kufahamu na kutambua ni kazi gani ianze kufanyika na ipi ifuate. Hivyo kama kweli umeuchoka umaskini jifunze kupanga vipaumbele kwa vitu unavyofanya kwa kuangalia nini kianze kufanyika, lini na kwa wakati gani.
3. Jifunze kuyaweka malengo yako katika nyakati.
Malengo uliyonayo ni lazima uyaweke katika nyakati kabla hujaanza kufanya, na nyakati hizi ni lazima uwe ni wakati uliopo na wakati ujao.
Jambo hili linahitaji maamuzi magumu, yaani amua kwamba jambo hili ni lazima nitafanya wakati huu au aumua jambo hili ni lazima nitalifanya muda fulani. Katika kipengele hiki ugopa sana tabia ya kugharisha kufanya kwani ndiyo inayoendelea kukuua taratibu bila wewe kujua.
4. Andika kila kitu ulichokifanya au unachotaka kufanya.
Kuandika mambo yako uliyoyafanya au unayotaka kufanya humpa mtu hamasa za kiutendaji kwani mara kwa mara anakuwa anakumbuka ni kitu natakiwa kufanya na kwa wakati gani? .
Ogopa kufanya mambo ya msingi kwa kukurupuka kwani hii ndiyo ambayo husababisha watu wengi kutokufanya maumizi sahihi. Hivyo kila nyakati jifunze kuweka kila kitu katika maandishi ili uweze kujijengea fikra thabiti.
5. Fahamua kile unachokitaka.
Maisha sio bahati nasibu bali maisha ni vile unavyotaka kuwa na muamuzi wa mwisho ni wewe, hivyo kaa chini na tafakari kwa makini ni nini hasa unachokitaka kisha uanze kuchua hatua stahiki juu ya jambo hilo.
Lakini pia ikumbukwe kufahamu kile unachokitaka pasipo kuchukua hatua za kiundeji ni sawasawa na bure, hivyo amua sasa kubadilika kwa kuchukua hatua za kiutendaji kwa kile unachokifanya.
Mwisho naomba nihitimishe kwa kusema ya kwamba endapo ukiyazingatia hayo yote niliyokwisha yaeleza jiandae kuishi maisha yenye tija katika hii dunia.
Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya