Mambo Ambayo Umekuwa Ukidanganywa Sana Kuhusu Pesa Na Uwekezaji.

Kati ya kitu ambacho kinatafutwa sana na wengi hapa duniani ni pesa. Pesa imekuwa ikitafutwa usiku na mchana karibu na watu wote. Hali hii imekuwa iko hivyo kwa sababu ya umuhimu wa pesa katika kutusaidia kufikia malengo yetu.
Lakini pamoja na pesa kutafutwa hivyo, bado watu wengi wamekuwa wana hadithi nyingi za uongo kuhusiana na pesa hata swala la uwekezaji kwa ujumla.  Kila inapotajwa pesa au uwekezaji wakati mwingine kumekuwa na uongo mwingi sana wa kupotosha.
Ni lengo la makala haya kukuwezesha kutambua mambo ambayo umekuwa ukidanganywa juu ya pesa na uwekezaji. Mambo hayo ni yepi? Fuatana nami katika makala haya mwanzo hadi mwisho tuweze kujifunza kwa pamoja:-
1. “Unahitaji pesa nyingi ili kuwekeza”.
Wengi wetu bado tunaendelea na fikra mgando za kuamini kwamba ili uweze kuwekeza ni lazima uwe na pesa nyingi. Kutokana na uongo huo, tumekuwa tukisubiri tupate mitaji na pesa nyingi ili tuweze kuwekeza.
Kwa taarifa yako huo ni uongo ambao umekuwa ukidanganywa. Kwa dunia ya sasa jinsi ilivyo, kitu kikubwa unachohitaji ni wazo na taarifa sahihi za mafanikio ili kuwekeza. Kama ni mtaji unahitajika sio lazima uwe mkubwa sana kama unavyofikiri.

Kwa hiyo kama umesimama na huwekezi kwa kisingizio cha kukosa mtaji, unajichelewesha mwenyewe. Zinduka kwenye huo usingizi na anza kutumia kidogo ulichonacho kufanya uwekezaji unao faa kwako. Naamini kipo kitu ulichonacho hata kidogo cha kukusaidia, hauwezi kukosa vyote.
2. “Uwekezaji ni hatari”
Jambo la pili ambalo wengi wamekuwa wakidanganywa sana kuhusu pesa na uwekezaji kwa ujumla ni kwamba, uwekezaji ni ‘risk’ kubwa sana. Nafikiri umeshawahi kusikia hadithi za namna hii sana kuwa uwekezaji ni hatari.
Kutokana na wengi kupokea hadithi za namna hii na kuzikubali kupelekea kutokufanya uwekaji wowote ule. Unajua ni kwa nini? Kwa sababu wameshaambiwa uwekezaji ni hatari na ni ‘ risk’ kubwa sana.
Huu ni uongo ambao umekuwa ukidanganywa kwa muda mrefu. Na kwa bahati mbaya umekuwa ukijisahau pia kwamba uwekezaji sio hatari kubwa sana kama unavyofikiri, ila unachangamoto zake na ni njia mojawapo nzuri ya kukufikisha kwenye uhuru wa kipesa.
3. “Mshahara ndio kila kitu”
Acha kuendelea kuugua na kuamini hadithi za kwamba wale wanaolipwa mshahara ndio kila kitu. Kama hicho ndio kilio chako na unaamini tosha kabisa kwamba eti kwa sababu wewe hukusoma na hulipwi mshahara basi maisha yako yameharibika.
Sikiliza nikwambie rafiki, maisha ni mipango. Jiwekee taratibu zako za kutengeneza kipato na jiamini zaidi, utafanikiwa. Kama unafanya kazi acha kuwadanganya wengine kwamba ukiwa na mashahara ndio uhakika wa mafanikio.
Mafanikio ya kweli hayaji kwa sababu ya mshahara unaolipwa. Mafanikio makubwa na ya uhakika yanakuja kutokana na mipango yako imara uliyojiwekea na kuifata kila siku.
Ukiangalia na kufuatilia hizo ndizo hadithi ambazo una danganywa sana kuhusu pesa na uwekezaji. Mengi yamekuwa yakisemwa sana kuhusu pesa na wekezaji kitu ambacho sio kweli.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Napenda pia kuchukua fursa hii kukukaribisha kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja na kwa ukaribu zaidi. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifutia na namba yako kwenda 0713 04 80 35 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,

Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel