Hii Ndiyo Kanuni Ya Mafanikio Iliyosahaulika Na Wengi.

Mafanikio hayatengenezwi na kanuni moja tu, bali ni mjumuiko wa kanuni za kimafanikio tofauti tofauti na hizi ndizo ziletazo mafanikio. Zipo kanuni za wazi kabisa za kimafanikio ambazo zinafahamika na wengi na zipo ambazo hazifahamiki.
Kwa mfano, kufanya kazi kwa bidii, kuwa na nidhamu, kutengeneza nguvu ya uzingativu, naweza kusema ni moja ya kanuni za mafanikio au misingi ya mafanikio ambayo inaeleweka na wengi kwamba ukiifata lazima ufanikiwe.
Hata hivyo inabidi ieleweke hivi, zipo kanuni nyingi za kimafanikio ambazo unatakiwa uzifanyie kazi sana ili ufanikiwe, na kwa bahati mbaya zipo ambazo huzijui au umezisahau kwa kutokujua lakini zipo na zinafanya kazi kwa matokeo makubwa.
Na mojawapo ya kanuni rahisi ya mafanikio ambayo wengi hawaijui au wameisahau, ni kanuni ya kuwa na shukrani. Inaeleweka kwamba kwa mtu yeyote ambaye ana shukrani, na huku akawa ni mtu wa kuchukua hatua kufanikiwa ni lazima kwake.
Sasa linakuja tatizo la watu wengi ni wabinafsi na hawana shukrani, kama unafikiri natania nianze na wewe, je, wewe ni mtu wa shukrani, je, wewe ni mtu wa kukumbuka kule ulikotoka na kushukuru hapo ulipo na kwa maisha uliyonayo.
Mara nyingi utakuta watu wengi hawana shukrani sana, si watu wa kukumbuka watu wale waliowasaidia na wapi, hata kama ni kwa kidogo na matokeo yake wanajikuta ni watu ambao wanaiweka kanuni hii pembeni na mwisho wake hushindwa kufanikiwa sana.
Kama nia yako ni mafanikio makubwa kweli, pia unatakiwa kuchukua shukrani kama mojawapo ya kanuni ya kimafanikio. Kila wakati unapochukua hatua za kiutendaji, lakini  hakikisha shukrani iwe karibu na kinywa chako kwa chochote kitakachotokea.
Kuna watu wana midomo kama ya ‘laana’ wanapochukua hatua, kwa mfano kufanya biashara ya aina fulani halafu wakapata hasara, midomo yao inakuwa inaongea mengi sana na kulalamika, sasa hii sio nzuri na haikusadii, shukuru kwa chochote.
Unaweza ukawa upo kwenye wakati mgumu shukuru kuna kitu cha kujifunza, unaweza ukawa umepata hasara kweli shukuru, hii ni kanuni ya kimafanikio na ambayo pia ni kanuni ya kiroho, pasipo kushukuru mambo yako hayawezi kwenda sawa saana.
Inawezekana sasa unajiuliza nashukuru kwa mambo yapi, hilo lisikupe tabu. Yapo mengi sana ambayo unaweza ukaanza kuwa na shukrani nayo lakini kwa kuanza tu, unaweza ukaanza na kushukuru kwa mambo haya na yatakusaidia sana kufanikiwa.

1. Shukuru kwa uhai ulionao.
Kwa sababu ile tu unaishi, kwa sababu ile tu umepewa uwezo wa kuishi unatakiwa kushukuru sana kwa hilo kwanza. Amka asubuhi na sali kwa kwa sababu umepewa uwezo wa kuishi na muumba wako na hicho ni kitu kizuri sana.
Kitendo cha kushukuru kwa uhai ulionao kitakupa nguvu hata ya kutenda mambo mengine makubwa maishani mwako ambayo moja kwa moja yatakusaidia kuweza wewe kufanikiwa kwenye maisha yako moja kwa moja.
2. Shukuru kwa afya yako.
Tofauti na kushukuru juu ya uhai ulionao, huna budi kushukuru kwa sababu ya afya uliyonayo. Sote tunajua afya ni msingi mkubwa sana wa mafanikio yako, hiyo ikiwa na maana kama huna afya ujue kabisa na mafanikio huna.
Shukuru kwa afya uliyonayo, kama kuna sehemu unaona unaumwa shukuru pia kwa sehemu zingine za mwili ambazo huumwi. Kwa kushukuru huku uponyaji una uwezo wa kusambaa na sehemu zingine za mwili kwa njia ambayo hata wewe huijui.
3. Shukuru kwa fursa zilizopo.
Tunaishi katika dunia kwa sasa ambayo fursa zipo nyingi sana. Nakwambia hivi ni kwa sababu tunaishi katika dunia ya habari. Kama  upo hapo na huoni fursa basi ujue kuna shida sehemu kwako au ‘umepigwa upofu’, hombre yako hayaoni.
Shukuru kwa sababu ya fursa zilizopo, ukishindwa kuchukua hatua fursa hii basi elewa ipo fursa nyingine kule, kikubwa ni kutuliza sana akili yako na kutumia fursa hizo za kimafanikio ziweze kukusaidia wewe na wengine wanaokuzunguka.
4. Shukuru kwa watu wanaokuzunguka.
Unalazimika kuwa na shukrani kwa watu wanaokuzunguka, watu hawa wanaweza kuwa ni ndugu, rafiki zako au jamaa zako lakini watu hawa wanamchango mkubwa wa kubadili maisha yako na inabidi uwatumie vizuri kukusaidia katika hilo.
Kama huna shukrani na watu wanaokuzunguka basi utakuwa unakosea na unajiweka katika wakati mbaya wa kutokuendelea kufanikiwa. Haujaja duniani wewe kama wewe,unaishi na kuzungukwa na watu, basi kuwa na shukrani na watu hao.
5. Shukuru kwa wakati mgumu.
Ni vyema pia ukawa na shukrani hata katika kipindi kigumu cha maisha yako. Kipindi kigumu cha maisha yako ni mwalimu mzuri wa kukufundisha na kukupa uzoefu wa wewe kukusaidia wewe kuweza kufanikiwa.
Unaweza ukawa hupendi sana nyakati hizi ngumu lakini kumbuka kipindi kigumu, hicho ndicho kinachokukomaza wewe na kukusaidia kuweza kufanikiwa. Unatakiwa uelewe nyakati ngumu hazipo kukuangusha bali kukusaidaia wewe kusimama kimafanikio.
Haya ndio mambo ya msingi unatakiwa uanze kuwa na shukrani nayo ili kanuni ya shukrani ifanye kazi kwako vizuri. Hata maandiko matakatifu yameandika juu ya shukrani. Wale walioshukuru walipokea muujiza zaidi maishani mwao.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,



Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel