Sababu Kubwa Inayokufanya Usianze Kuchukua Hatua Ni Hii…
Thursday, June 9, 2022
Moja ya sababu kubwa inayopelekea watu wengi kuahirisha mambo na kushindwa kuchukua hatua ni kule kufikiri kuna vitu havijakamilika katika kulifanikisha jambo hilo. Mtu anakuwa anaahirisha kwa sababu anakuwa anaona bado hajawa tayari kufanya jambo hilo kabisa.
Uelewe hivi, ni jambo zuri kufanya kitu chako ukiwa umekamilika kwa asilimia mia moja. Hata hivyo hiyo isiwe sababu ya wewe kutokuanza, unaweza ukaanza kwa hali yoyote uliyonayo hata kama unajiona hujakamilika sawa sawa.
Usiwe na wasiwasi juu ya kuanza jambo fulani huku ukiwa umekamilika kwa asilimia mia moja, kitu cha kwanza unachotakiwa kujua ni juu ya wewe kuanza. Fanya ufanyalo na uhakikishe umeanza kufanya jambo lako na usisite hata kidogo kuanza.
Kwa muda ulionao, kwa chochote kile ulichonacho, anza. Usisubiri ukamili wa jambo lolote ule ndio uanze. Usijiweke kwenye mtego wa kuahirisha kwa sababu ya kuanza. Kikubwa anza na kile ulichonacho na hapo ulipo na usisubiri kitu.`
Kama ukitaka uwe kamili kila kitu ndio uanze kufanya hicho unachotaka kufanya, hebu jiulize utajifunza nini kwenye safari ya mafanikio yako? Endelea kufanya huku ukiwa unajifunza na utafika muda utayafikia imafanikio yako kwa kiasi kikubwa.
Watu wengi ikiwa pamoja na wasomi mambo yao yanashindwa kukamilika au kufanyika kikamilifu kwa sababu tu ya wao wenyewe kutaka kufanya mambo yao wakiwa kamili kwa kila kitu, nikiwa na maana ni watu wa kutafuta ukamili sana.
Naomba labda nikwambie hivi, hata wale watu unawaona wamefanikiwa sana, hawakuanza wakiwa na kila kitu, walianza kidogo na vile walivyonavyo, ila kilichowafanya wakawa hivyo ni kwa sababu ya wao wenyewe kujifunza na kukua.
Ukikubali kuendelea kufanya huku ukijifunza na kukua, itafika muda hata kama ulianza na kidogo sana lakini nakupa uhakika utaweza kufanikiwa na kufika mbali kimafanikio, kwa nini, kwa sababu umeamua kufanya pasipo kujali ukamili.
Ili uweze kuondokana na hali ya kuahirisha mambo, acha kabisa kusubiri uwe kamili kwa asilimia zote, wewe fanya hivyo hivyo na utafika muda utaweza kufanikiwa katika hilo na ndoto zako zitatimia na kuwa kweli.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com