Mbinu Kumi Muhimu Za Kufanikiwa Kipesa Na Maisha Kwa Ujumla.
Friday, June 24, 2022
Maisha ni mjumuiko wa mbinu na kanuni mbalimbali ambazo ukizitumia ni rahisi kukuwezesha kufanikiwa sana. Mafanikio hayaji kwa siri moja tu, zipo siri au mbinu nyingi ambazo ukizitumia zitakupa mafanikio ya moja kwa moja.
Kwa kutumia mbinu hizo unaweza ukafanikiwa kipesa au unaweza ukafanikiwa kwa maisha ya nje iwe uongozi au vyovyote vile. Kupitia makala haya naomba nikwambie mbinu muhimu ambazo ukizifanyia kazi zitakufanikisha kufanikiwa.
1. Kuwa na maono tu ya kile unachotaka kukifanya hiyo peke yake haitoshi unatakiwa kuongeza imani na moyo wa kusonga mbele. Kwa maneno mengine bila maono, imani sahihi ya mafanikio na moyo wa kuweza kusonga mbele huwezi kufika popote.
VISION + FAITH + COURAGE= SUCCESS
Yapo maono ambayo kwako na kwa wengine yanaonekana kama ndoto yaani maono yasiyotimia. Maono hayo ili uweze kuyafikia lazima uwe na imani na moyo wa kusonga mbele hata kama unahofu yaani ‘courage.’ Ukiwa na vitu hivyo utafanikiwa.
2. Kaa tayari kujiandaa na kitu chochote kinachoweza kujitokeza kwenye maisha yako ya kiuchumi. Maisha yanabadilika, uchumi ulionao unaweza ukawa bora sana, lakini jiulize kesho mambo yakibadilika unafanyaje? Umejiandaa na mabadiliko hayo?
Unatakiwa kujifunza kukaa tayari kwa nyakati na mabadiliko yoyote yale ambayo yanakuwa yanajitokeza kwenye maisha yako. Usiyumbishwe na mabadiliko, bali jiandae na mabadiliko yanayoweza kutokea kwako.
3. Haijalishi utakulia katika mazingira yapi, lakini msingi mmojawapo mkubwa wa mafanikio ambao unatakiwa kuujenga na utakusaidia sana ni ukweli/truthful na ukarimu/honest. Hii ni misingi muhimu sana ya mafanikio yako endelevu.
Watu wengi kwa bahati mbaya sana wanalelewa katika uongo mwingi, wanatengeneza kipato kwa njia ya uongo, ni jambo ambalo ni hatari sana katika kujenga mafanikio ya kudumu. Jifunze ukweli na ukarimu utakusaidia sana.
4. Kila mtu ndani yake respeto anajua au hajui lakini amebeba watu hawa, mtu maskini, mtu tajiri, mtu mkweli, mtu mwongo, mtu shujaa na jasiri, mtu mnyonge na dhaifu na aina nyingine ya watu. Hawa ni aina ya watu walio ndani mwa kila mtu.
Hapa ni uamanuzi wako wewe mwenyewe ni ubebe mtu yupi na ambaye utaamua kumtumia ili akusaidia kufanikiwa. Mtu yeyote unaweza ukatoka naye ni swala la kuamua sifa ama ‘character’ ipi unataka kukua nayo kwenye maisha yako yote.
5. Kama pesa huwezi kuziona kwenye akili yako, kama pesa huwezi kuziona kwenye kichwa chako, basi hata mikononi mwako pesa huwezi kuziona. Pesa unalazimika kwanza kuziona kwenye akili yako kabla hazijakufikia mikononi mwako.
Wengi ambao wanakosa pesa si kwamba pesa hizo hawazioni mikononi mwao bali hata kwenye akii zao hawaoni pesa hizo. Anza kuona fursa za pesa akilini mwako kwanza tuone kama pesa utazikosa mikononi mwako tena.
6. Usisubiri umri uende ndio uanze kutafauta hatma ya maisha yako, usisubiri miaka iende huku ukiendelea kutafuta kazi moja na kuelekea nyingine. Hakikisha una biashara yako iliyosimama, hakikisha una maisha yako yanayojitegemea huku ukiwa bado kijana na mapeema, hiyo itakusaidia sana.
Hatma ya kesho yako amua kuitegeneza leo hata kama ni kwa tabu sana, lakini tafadhali itengeneze hatma ya kesho yako leo leo hata kama ni kwa tabu. Kesho itafika na mambo yanaweza yakabadilika utapata shida sana kama hukuwekeza kujiandaa mapema. Amua kuitengeneza kesho yako nzuri leo hata kama ni kwa gharama sana.
7. Kama leo hii ikitokea huna pesa, huna kazi, huna pa kulala, huna chakula ni kitu gani ambacho utakwenda kufanya? Utachanganyikiwa au utahaha au ni kitu gani ambacho utafanya? Fikiria kidogo halafu ujijibu mwenyewe.
Najua wengi watakimbilia kusema kwamba watakwenda kutafuata kazi na kufanya. Jibu lolote utakalolitoa hiyo inayoonyesha ni jinsi ulivyokuwa ‘programudi.’ Kwa aliye ‘programudi’ tokea awali kuwa mjasiriamali atasema anaenda kufanya biashara.
8. Wazazi na walimu wanasisitiza sana mtoto asome vizuri, apate elimu bora. Kitu ambacho wanasisitiza hapo ni ule ulinzi na hawasisitizi uhuru. Kitu kizuri kuliko vyote hapo ni uhuru na sio ulinzi kama wengine wanavyofikiri.
Kitu cha kufanya ni kubadili mtazamo wako kutoka kwenye kutafuta ulinzi na kutafuta uhuru wa kipesa. Kwa bahati mbay au nzuri kwa chochote unachokitafuta sana na kitu hicho kitakupelekea kukosa kitu kingine, angalia ni kipi muhimu sana kwako.
9. Lipo kundi kubwa sana la watu ambalo linafata mipango iliyokufa, mipango hiyo inaweza ikawa ya wazazi, ndugu au rafiki. Kwa nini nasema mipango iliyokufa nikiwa na maana, kama unafata mipango ya mtu aliyeshindwa kifedha na wewe utashindwa tu na hiyo inakuwa ni sawa na kufuata mpango ambao umekufa tayari.
Kila wakati fata mipango imara ya mtu aliyefanikiwa kifedha na wewe utafanikiwa. Ikiwa lakini utafata mipango ya mtu aliyeshindwa kimafanikio na wewe utashindwa tu. Jiulize sasa unafata mipango iliyokufa au unafata mipango iliyo hai? Ukifata mipango ya mtu aliyeshindwa enelwa unafata mipango mfu, mipango iliyooza.
10. Hebu jiulize, unawezaje kubadilisha fikra za mtu ambaye yeye tokea anakua amefundishwa kwamba ili uwe na maisha mazuri ni lazima kwanza uwe na kazi. Kubadilisha fikra kama hizi ni kazi kubwa na inayotaka uwe na moyo mkubwa ili fikra hizi ziweze kubadilika, hapa ndipo tatizo la wengi lilipo kwa sababu ya hilo.
Ndio maana hata iweje wapo watu ambao hawawezi kuwa wafanyabiashara kwa sababu, ni watu ambao wao wanajua jinsi ya kupokea mshahara na si kitu kingine. Kwa hiyo kama wewe unaona una damu ya ujasiriamali kazana vivyo hivyo, waache ambao hawataki kuwa wajasiriamali utawauzia bidhaa wewe.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com