Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuondokana Na Majuto Uliyonayo Na Kuishi Maisha Ya Amani Na Furaha.

Wengi wetu huwa tunajuta sana. Mara nyingi tunapokumbana na kushindwa kwetu au mambo yetu kukataa kwenda kama tulivyotarajia, huwa tunajuta sana. Nini yaweza kuwa hasa sababu ya kujuta kwako sana na pengine huweza kupelekea wewe mwenyewe kuanza kujiona kama hufai vile.
 
Kujuta huweza kujitokeza pale ambapo hukutenda itakiwavyo kwa kile ulichokuwa ukikifanya. Kujuta sio kubaya kama ni kwa ajili ya kurekebisha makosa. Kuyajua makosa hayo ina faida kwa maana kwamba sasa unaweza kubadilika na kuwa tayari kwa ajili ya maendeleo au kufanya vizuri zaidi. 

Huku ni kujuta kwenye kujenga na kwa hali hiyo hatupaswi kuita hali hii kujuta. Kama tutajilaumu kwa kushindwa, bila kujali kama ni kosa letu au hapana, hapo ndipo tunapoita kujuta. Kujuta siyo kule kujua kwamba, tumekosea na pengine ni uzembe, lakini tukawa tayari kujifunza.

Kihoro cha mawazo kina uhusiano na mambo yaliyopita. Ili mawazo hayo yaweze kudumu hayana budi kubaki ndani ya moyo wako. Kila siku unayoishi, yaani leo, ndiyo siku yako kubwa ya kujisahihisha. Ukiruhusu mawazo yako yakutawale, basi utakuwa umejilimbikizia kikwazo kikubwa dhidi ya maendeleo yako.

Kwa kadiri utakavyoendelea kujuta sana bila kujifunza kitu, ndivyo utakavyojikuta maisha yako unazidi kuyaharibu. Hii inatokea kwa sababu unakuwa hufanyi kitu kipya, unakuwa umeganda kwenye kujuta tu. Unawezaje kupambana na majuto haya unayokutana nayo mara kwa mara katika maisha yako na ili yasikuumize tena? 

1. Kuwa na muda wa maamuzi

Kufikia sasa utakuwa umeshajielewa wewe ni nani na unataka kuzoea nini badala ya kile ulichokuwa umekizoea. Ukishajua unachokitaka fanya kile ambacho unapaswa kufanya kama vile, kubadilisha imani. Njia yenye nguvu ni kuvifanya vitu ambavyo una uwezo wa kuvifanya. Unachokifanya leo kinaathiri maisha yako ya baadae na kitakusaidia usijute baadae.



2. Jiulize sana maswali.
 
Kile ukifanyacho ni kupambana kwa ajili ya kubadili unavyojisikia. Unataka kujisikia vizuri kwa nini uhisi majuto ndani yako na kufadhaika. Kama una utashi wa kweli wa kutaka kuondokana na kujilaumu, lazima upitie zoezi zima la kujiuliza maswali mazito.

Hii ni aina mojawapo ya kubadili mwelekeo wa ubongo wako. Kwa yale yote unayoyajua unaweza kuwa unayaalewa mambo pengine kimakosa. Endelea kujiuliza maswali ili kuweza kugundua mambo ambayo ulikuwa hujayaona na ambayo yanakufanya uumie na kujuta.

3. Badilisha picha katika mawazo yako.

Mawazo kuhusu mwenendo wako mbaya au upumbavu wako husababishwa na picha ambazo uliziunda ndani ya akili yako.  Unaendelea kujiadhibu, kwa kila wakati kwa kuziona taswira na kukurudisha nyuma ulikotoka. Unavyozidi kukumbuka ya kale, ndivyo unavyozidi kuleta majuto.
Una udhibiti juu ya yale tu yanayojionyesha kwenye fikira zako. Unaweza kufanya hivyo kwa kupandikiza mawazo mapya na mazito juu ya yale ya zamani, ambayo umeyagandisha kwenye ubongo wako. Inahitaji nidhamu na kujitoa mhanga, tena ni jambo la maana ili kujiondoa kutokana na uozo uliopita.

4. Geuka na fanya mabadiliko

Kama ulichokuwa umekifanya kilikuwa kibaya achana nacho. Badilisha mwelekeo. Jipe ahadi mwenyewe kwamba hutarudia tena. Jisamehe kwa ujinga wako. Kama umewakosea wengine au umewaumiza waombe msamaha, kisha songa mbele.

Fanya kazi na fanya vitu ambavyo vitakufanya ujisikie vizuri na kurudisha kujiamini kulikokuwa kumepotea. Hujacheleweshwa kuanza upya wala usijali kuhusu umri wako. Daima kuna kitu ambacho unaweza kukifanya ili kuyaweka maisha yako na ya wengine sawa.

Kumbuka, ni lazima wote tuathiriwe na aina mbili za maumivu, maumivu ya nidhamu na maumivu ya kujuta. Tofauti ni kwamba nidhamu ina uzito kidogo na majuto yana uzito mkubwa. Hivyo, ndivyo unavyoweza kuondokana na majuto uliyonayo na kuishi maisha ya amani na furaha.

Nakutakia mafanikio mema katika maisha yako, karibu sana na endelea kutembelea mtandao huu wa kwa kujifunza mambo mazuri yatakayokuwa yanakujia.

TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE.

Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel