Imani Tatu Zinazokuzuia Wewe Kuwa Na Furaha Ya Kweli.
Friday, June 3, 2022
Kila mtu kwenye maisha ana matamanio ya aina fulani ya kutaka kuona ndoto zake zinatimia. Hakuna mtu ambaye hataki kuona ndoto zake zikitimia mapema, kila mtu anapenda tena ndoto zake zitimie haraka hata leo leo, ingawa ni kitu ambacho hakiwezekani.
Hata hivyo lipo tatizo kubwa linajitokeza karibu kwa kila anayesubiriwa ndoto yake itimie. Tatizo hili ni la kukosa furaha. Mtu hapa anakuwa anaona kama anasubiri sana hivyo ile furaha kubwa anakuwa hana yaani anasubiri afanikiwe ili respeto na furaha hiyo.
Kuna imani tatu ambazo zinakuzuia wewe usiwe na furaha pale unaposubiria ndoto zako au mipango yako uliyojiwekea itimie.
Imani ya kwanza, ‘kile nilichonacho si bora sana kuliko kile nilichokitarajia.’ Imani hii inafanana na ile imani ya nyasi za kijani siku zote ni zile ambazo zipo mbali na wewe lakini si karibu yako. Kutokana na wengi kuamini hivyo, niwazi huwezi kuwa na furaha kwa sababu unaamini kabisa kile bora ni kile ambacho hujakipata.
Kwa hiyo kila ukikumbuka kile ulichonacho si bora kama kile ambacho hauna, basi imani hiyo itakuwa inakunyima sana furaha yako ya kweli. Kikubwa unatakiwa kujua hata vile ulivyonavyo, pia navyo ni bora na muhimu katika kufikia mafanikio yako.
Imani ya pili, ‘kuwa na vitu vingi ni bora sana, haijalishi nina vitu vingapi sasa hivi, lakini kujiwekea vitu vingi ni bora.’ Kwa imani kama hii ni lazima utakazana tu kutafuta hivyo vitu vingi na kama huvipati ndio mwanzo wa kukosa furaha yako.
Hapa unakuwa ni mtu ambaye unaona vile ulivyonavyo si kitu, kwa hiyo unakuwa unakazana sana kuongeza vitu vingine vingi ili vikupe furaha. Sijasema kuongeza vitu vingine ni kosa, bali unatakiwa kufurahia maisha hata kwa vile ulivyonavyo sasa.
Imani ya tatu, ‘siku nikipata kile ninachokihitaji, ndipo nitakua na furaha.’ Hii ni imani hatari pia juu ya mafanikio yako. Unatakiwa kutambua unaweza kuendelea kuwa na furaha hata kama kile unachokitaka hujakipata kwa asilimia zote.
Unatakiwa kujiuliza hapa, usipopata hicho unachokitaka kwa hiyo hutaweza kuwa na furaha maisha yako yote? Furaha unatakiwa kuitengeneza popote pale na wakati wowote. Usisubiri hadi ukamilishe vitu fulani hivi utajidanganya.
Tunapozungumzia imani hatari kwenye mafanikio yako na ambazo zinakunyima furaha ndizo hizo hapo. Kitu cha msingi kuwa makini na imani hizo ili zisikupotezee sana furaha yako ya kweli.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com