Huu Ndio Uongo Unaokuzuia Ushindwe Kuchukua Hatua.

Uwe unajua au hujui unatakiwa kujua kuna wakati upo uongo unaojijaza mwenyewe na kwa bahati mbaya sana uongo huo  ndio unaokuzuia ushindwe kuchukua hatua za kuelekea kwenye mafanikio yako uliojipangia kuyafikia
Inawezekana unajiuliza inawezekanaje na kivipi mtu ukajijaza mwenyewe uongo, ndio inawezekana kabisa kwamba ukajidanganya mwenyewe na ukajipoteza kutokana na mawazo ambayo unajisemea mwenyewe kila wakati.
Hapa kupitia makala haya nataka nikuonyeshe uongo ambao unajiambia wewe mwenye na kwa uongo huo unakuzui wewe kuweza kuchukua hatua za kufikia mafanikio yako. Je, uongo huo ni upi unaojiambia?

1.”Siko tayari kufanya jambo hili kwa sasa.”
Kuna watu ambao wanajidanganya katika hili nakuona kile wanachotakiwa kukifanya kwa sasa hawako tayari, nikiwa na maana watu hawa wanakuwa wanadai maandali mengine zaidi bado yanahitajika ili waweze kuchukua hatua.
Matokeo yake watu hawa huendelea kujiandaa wee na mwisho hushindwa kuchukua hatua kabisa. Sasa huu ni uongo ambao wengi wanajidanganya, wakati unatakiwa kuchukua hatua hata kama unajiona hauko tayari lakini wewe chukua hatua.
2. “Natafuta wazo bora zaidi.”
Moja ya kizuizi kinachowazuia watu wengi kushindwa angalau kuchukua hatua ya kwanza tu kwa kile wanachokifanya ni kutokana na wao kuendelea kutafuta wazo bora zaidi la kibiashara badala ya kulifanyia kazi lile walilonalo.
Utakuta mtu ana mawazo mazuri tu ya kibiashara lakini unaona mtu huyo anaendelea kutafuta wazo lingine bora na kuacha kutumia hata lile wazo walilonalo. Huo ni uongo mwingine wa kuamini lipo wazo bora zaidi la kufanyia kazi.
3. “Nimeshachelewa kwenye mradi huu.”
Kati ya mojawapo ya wazo linalopoteza wengi ni kule kwa wengine kuamini mradi wanaoufanya tayari wameshachelewa wakiwa na maana kwamba mradi huo tayari unafanywa na watu wengi na jambo ambalo si sahihi.
Kuendelea kuwa na mawazo haya ni kujidanganya tu, hakuna kitu ambacho umechelewa wewe kufanya kwa sehemu yako na weka juhudi vya kutosha na kuhakikisha hadi unaweza kufanikiwa vya kutosha.
Kwa kumaliza makala haya, tambua huo ndio uongo ambao wengi wanajidanganya na unawafanya washindwe kuchukua hatua za kufikia mafanikio yao.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel