Sababu Nne (4) Kwanini Unapata Pesa Lakini Huna Maendeleo.

Najua unafahamu fika kuwa kuna baadhi ya watu umeanza nao kazi au biashara fulani lakini kila ukiangalia maendeleo yao mara nyingi huwa ni ya muda mfupi au kokesekana kabisa kwa mafanikio kwa watu hao na ilihali watu hao wanapesa nyingi.

Pamoja na kuwepo kwa fedha nyingi kwa watu hao lakini watu hao hawana mafanikio, je unajua ni wapi ambapo watu hao hukosea? naomba ufatane nami nikueleze sababu ambazo hupelekea watu hao kutokuwa na maendeleo.


1. Kutokuwa na malengoThabiti.

Kutokuwa na  malengo ndo mzizi mkuu wa kukosa maendeleo. Kutokuwa na malengo ni sawa na kuwa na nauli huku ukiwa hujui ni wapi unapotaka kuelekea. Kama ilivyo mfano wa kuwa na nauli iko vivyo hivyo hata katika maisha ya kimafanikio.

Agalia  watu wengi wanatafuta pesa kwa bidii lakini kwa sababu watu hao hawana malengo thabiti mwisho wa siku wanaishia kuzitumia ovyo pesa hizo kitendo hiki kinawafanya watu hawa wanaendelea kuwa maskini miaka nenda miaka rudi.

Hivyo ndugu yangu ili uweze kujipatia maendeleo yako unatakiwa kuwa ni mtu wa kupanga malengo kisha kuyatekeleza kwani ukiwa hauna malengo utaishia kulalama kwamba kila ukipata pesa hakuna cha maana unachofanya.

2. Kutaka kufanya kila kitu kwa wakati moja. 

Ni kweli  una pesa na una hamu ya maendeleo, lakini huna malengo thabiti yanayokuongoza wewe katika matumizi yako ya pesa. Watu wenye tabia hii huwa ni watu wenye kutapatapa  yaani wewe unakuwa ni mtu wa kutazama watu wengine.

Kama hunielewi hapa kwa uzuri sikiliza, ukiona mtu kanunua kiwanja nawe utanunua, ukiona mtu amejenga nawe utataka kujenga mwisho wa siku utajikuta huna hata kitu cha maana ulichofanya na pesa imeisha yote na huku ukibaki unajishangaa.

Siku zote kuwa ni mtu wa kuchagua jambo moja moja katika utekelezaji kwani tabia ya kuiga kutoka kwa wengine itakufanya uendelee kuwa mtumwa wa umaskini. Maisha yako ni maisha yako tu, jifunze kutliza akili na kufanya jambo moja kwanza.

3. Kutoa zaidi kuliko uwezo wako

Si vibaya kutoa lakini, miongoni mwa tabia ambayo inawatafuna watu wengi wenye kiwango kikubwa cha fedha ni vile walivyo wazuri katika sura la kuonesha uwezo wao wa kifedha mbele ya watu wengine.

Hivi umewahi kwenda mahali fulani kisha kukawa na utoaji/ uchangiaji wa jambo fulani? je watu ambao wana fedha huwa wanakuwaje katika suala hili? jibu baki nalo.

Kama nilivyosema, sina maana ya kwamba kutoa ni kubaya la hasha ila maana yangu ni kwamba kila wakati jifunze kutoa kutokana na kiwango ulichonacho, kama wewe ni wa moja basi utoe moja, maana wa moja akivaa mbili huku ni kujitengenezea nyumba ya umaskini.

4. Kuwa na matumizi ya hovyo.

Ni kweli una matumizi ya hovyo kwa vile huna malengo basi hata kama una pesa ambazo si nyingi lakini utaziona nyingi sehemu ya kutembea utapanda bajaji kisa una buku ambayo ipo ipo tu mfukoni na imezibaa.

Pengine umeshiba lakini una 200 mfukoni ambayo haina kazi utanunua karanga huna shida ya nguo lakini una laki mfukoni isiyo na malengo utanunua shati kwa system hiyo utaishia kuwa na pesa nyingi lakini utakosa maendeleo kwa sababu unanunua vitu ambavyo havikuwa katika mipango yako.

Kwa leo naomba niweke nukta kwa kusema ya kwamba kama utaendelea kuyabeba mambo hayo katika mikono yako basi neno mafanikio utaendelea kusoma na kayasikia tu. Weka mipango au mikakati ya kukutoa hapo kikamilifu na utafanikiwa.

Ndimi: Benson Chonya


Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel