Mbinu Muhimu Itayokufanya Uondokane Na Msongo Wa Mawazo.

Msongo wa mawazo ni ile hali ambayo humpata mtu kisha kumpelekea mtu huyo kuwa na mawazo mengi kupita kiasi. Mawazo haya yanaweza kuwa chanzo chake mahusiano, kazi,elimu, magonjwa, biashara, fedha na mengineyo mengi.

Pamoja na kuweko kwa vyanzo hivyo au visababishi hivyo vya msongo wa mawazo inaelezwa kuwa msongo wa mawazo mara nyingi husababishwa na mahusiano, usigune huo ndio ukweli, pia leo sipo kwa ajili ya kuzungumzia msongo wa mawazo utakanao na mahusiano bali nipo hapa kuzungumzia namna ambavyo utaweza kuondokana na msongo wa mawazo.

Nataka kuzungumzia namna ya kuondokana na msongo wa mawazo kwani athari ya kuwa na msongo wa mawazo ni kubwa mno. Tumekuwa tukiwaona watu wakishindwa kufanya kazi wazifanyazo kwa ufanisi eti tu kwa sababu watu hao wana msongo wa mawazo.


Lakini athari iliyo kubwa kupita zote wapo baadhi ya watu ambao huchukua hata maamuzi ya kujaribu kujiua kwa sababu tu mawazo  waliyonayo yamewazidi  akilini mwao.  Lakini athari nyingine ya msongo wa mawazo ni kwamba ni chanzo cha magonjwa mbalimbali. 

Swali ambao huwa najiuliza hivi ni kwa nini watu hao hufikia uamuzi huo wa kutaka kujiua? Hivi ni kweli watu hao hawajui namna ya kuweza kuondokana na hali hiyo ya msongo wa mawazo? . Kwa majibu yangu ya haraka haraka nikagundua yawezekana ni kweli watu wengi hawajui namna ya kuondokana na msongo wa mawazo.

Kwa kuwa hawajui basi naomba niwape mbinu hii maridhawa ambayo itawafanya watu hao waweze kujifunza hapa namna ya kuondokana na msongo wa mawazo kama ifuatavyo: 

·  Unatakiwa kutafuta majibu ya changamoto iliyokufanya uwe katika msongo wa mawazo.

Msongo wa mawazo sababu yake kubwa hutokana na changamoto fulani iliyokukabili katika eneo lako fulani. Hivyo kila wakati usiwe ni mtu wa kunung'unika, au kuamua kuchukua uamuzi fulani ambao ni mbaya utakaokufanya kuyagharimu maisha yako kwa namna moja ama nyingine, bali jifunze kutafuta majibu chanya yatakayokufanya uondokane katika hali  hiyo ya msongo wa mawazo.

Kutafuta majawabu ya changamoto zinazomkabili mtu, humsadia mtu huyo kwa namna moja ama nyingine kutengeneza amani ya moyo, na mtu anapokuwa na amani ya moyo huwa ni mtu chanya kwa kuwa mara nyingi hujiwekeza katika mawazo mazuri yatakayomsadia kufanya mambo yenye tija na si vinginevyo.

Mwisho naomba nitamatishe kwa kusema mara zote epuka msongo wa mawazo kwa kuzingatia njia hii ambayo nimeieleza hapa kwani msongo wa mawazo huwa una athari kubwa sana katika maisha ya kila siku kimwili na kifkra pia.

Kwa leo naomba niishie hapa tukutane tena panapo majaliwa,

Ndimi: Benson Chonya.

Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel