Jambo Hili Ni Muhimu Sana Katika Ukuaji Wa Biashara Unayoifanya.
Wednesday, June 22, 2022
Katika biashara yeyote ile unayoifanya ni lazima uweze kujifunza mbinu maridhawa zitakazokufanya uweze kukua katika biashara hiyo, hii ni kwa sababu moja kati ya changamoto kubwa ambayo inawakumba wafanyabiashara wengi kutofanya vizuri katika biashara wanazozifanya ni kwamba wanashindwa kujifunza mbinu mpya za kibiashara zitakazowasaidia wao kuweza kukua katika biashara husika.
Soko maalumu, hii ni kanuni muhimu sana katika biashara kwani ndiyo utambulisho wa biashara unayoifanya, huenda ukawa bado hujanielewa ipo hivi unapofanya biashara ni lazima uweze kutengeneza alama, na alama hizi ziwakae wateja wako akili mwao.
Kama na wewe ni miongoni mwa watu watu ambao wanakumbwa na sakata hilo basi nakuomba usipepese hombre mahala pengine bali endelea kusoma makala haya kwani leo nimekusogezea makala muhimu sana kwako itakayokufanya wewe uendeleee kufanya vizuri katika biashara ambayo unaifanya.
Tunafahamu fika ulimwengu wa sasa ni ulimwengu wa biashara hivyo bila kujiongeza katika biashara tunayoifanya tutashindwa kufikia malengo yetu ya kibiashara, hivyo ndugu yangu kwenye biashara yeyote ile ili uweze kufanikiwa ni lazima ujifunze kujitengenenezea soko lako maalamu.
Pia ninapozungumzia alama nina maana ubobezi katika eneo fulani, yaani kwa mfano mtu akisikiaa neon “kwa Beny fashion” basi ajue moja kwa moja huyu anahusika na nini. Kama wewe ni muuzaji wa viatu vya dukani basi hata jina lako likitamkwa mbele ya masikio ya watu basi watu hao wajue fika wewe ni muuzaji wa viatu.
Kufanya hivi ndiyo kitendo ambacho huitwa kutengeneza soko lako maalum. Pia kitendo hiki kinapochukuliwa hatua stahiki ndicho kinawafanya wafanyabiashara wengi waliofanikiwa waendelee kuyakumbatia mafanikio ya biashara zao.
Hivyo mpenzi msomaji wetu kila wakati ni lazima uweze kujifunza kutengeneza soko lako maalumu katika kila eneo unalolifanyia kazi, ni lazima wateja wako watambue kuwa wewe ni mbobezi zaidi katika eneo gani? Kitendo hiki kitawafanya wateja wako wasambaziane taarifa kwa haraka sana kwa kile unachokifanya.
Lakini pia ni lazima ikumbukwe ya kwamba neno mafanikio sio uchawi kama wengi wazaniavyo, bali ni matokeo ya vitu vidogovidogo ambavyo wengi huvipuuza. Hivyo kuanzia sasa jifunze kuchua hatua kwa vitu vidogo vidogo ambayo unaona fika havina mchango wowote wa kufanikiwa kwako, kwani vitu hivyo ndivyo vitavyokupa mafanikio unayoyataraji.
Hivyo kila wakati ni vyema ukajifunza kujitengenezea soko lako maalum ili uweze kufanikiwa katika biashara.
Ndimi; Afisa Mipango: Benson Chonya