Katika Maisha Acha Kubweteka Na Jambo Hili.
Thursday, June 2, 2022
Hapo zamani za kale wakati nasoma shule ya msingi nilikuwa ni mvivu sana wa kujisomea hasa pale ninapokuwa nyumbani, baba yangu aliigundua tabia yangu hivyo alipanga kudhibiti tabia hiyo mara moja.
Aliamua kuanzisha utaratibu wa kunipa maswali ya hesabu taribani 30 kwa kila siku , hii yote ulikuwa ni utaratibu wake ambao aliona utanisadia kuongeza uwezo wangu wa kufanya katika somo la hesabu lakini pia ili niweze kuongeza uwezo wangu wa kujisomea hasa pale ninapokuwa nyumbani.
Miongoni mwa vitu ambavyo huwa sivisahau mpaka leo hii kutoka kwa baba yangu ni pamoja na adhabu alizokuwa ananipa hususani pale nilipokuwa nakosa hesabu zile alizokuwakuwa ananipa, hata niwe nimepata asilimia 95 nilikuwa nachapwa vibako kama mtu aliyepata sifuri.
Yeye alikuwa hangalii hesabu nilizopata, bali yeye alikuwa anangalia zile nilizokosa zaidi, na mara baada ya adhabu ya viboko, baba alikuwa ananiuliza ni kwanini nimekosa zile hesabu?, mwanzoni niliona baba ananionea kwa kunipa adhabu za viboko kwa kukosa asilimia tano pekee.
Ila kadri siku zilivyozidi kwenda nilikuja kumuuliza baba ni kwanini alikuwa ananifanyia vile?
Baba alinimbia nilifanya vile ili kukufundisha somo muhimu sana katika maisha ambalo halina uhusiano na hesabau zile, na somo hilo ni la muhimu sana katika maisha yetu na somo hilo linaitwa kubweteka. Unajua katika maisha watu hufurahia zaidi yale waliyokamilisha pekee huku wakiyasahau kabisa yale ambayo hawajayafanya au kuyakamilisha.
Pia kitendo cha kuyafurahia yale ambayo umeyafanya na kujiona wewe ni bora zaidi hukufanya uzidi kubweteka na kuachana na yale unayoyakosea katika maisha, hivyo mwanangu katika maisha haya unatakiwa kukumbuka ya kwamba yale uliyoyapanga na kuyakamilisha ni jambo jema sana, ila kama unataka kuwa bora zaidi ya hapo ulipo sasa unatakiwa kushughulika na yale machache yalikuwa ni vikwazo ambayo yamekufanya ushindwe kufanya vizuri zaidi.
Mara baada ya kuongea hayo nilimshukuru sana baba yangu kwa kunipa mwangaza mpya ambao utanisadia mimi kwa namna moja ama nyingine kuweza kupiga hatua za kimafanikio.
Hivyo ni amani yangu kubwa hata wewe ambaye unasoma makala haya utaacha kushughulika na yale mazuri pekee unayofanya bali utaanza kushughukika na yale ambayo ni kikwazo kwako yanayokufanya ushindwe kuwa bora zaidi.
Mpaka kufika hapo sina la ziada naomba nikutakie siku njema na mafanikio mema.
NDIMI: Afisa Mipango Benson Chonya.
0757909942.