Mambo Matano Ambayo Watu Wenye Mafanikio Hawapotezi Muda Wao Kuyafanya.

Yapo mambo ya wazi ambayo watu wenye mafanikio hawayafanyi kabisa kwenye maisha na kwa kutokufanya mambo hayo huwapeleka kila siku kuendea kuchanja mbuga ya kukaribia mafanikio yao kwa ukaribu sana.
Ukilinganisha na watu ambao hawana mafanikio, wao hufanya sana mambo hayo lakini watu wenye mafanikio hawafanyi mambo hayo na wala hata hawashuguliki nayo sana kuyafikiria kuyafanya na ndio siri ambayo huwaweka karibu na kufanikiwa.
Je, unataka kujua ni mambo gani ambayo watu wenye mafanikio hawafanyi na kwa kutofanya ndio siri kubwa inawapa na kuwasogeza kwenye mafanikio makubwa. Twende pamoja kujifunza kupitia makala haya muhimu kwako.

1. Hawapotezi muda wao kuwa na watu hasi.
Hata siku moja watu wenye mafanikio hawapotezi muda wao wa thamani kuwa na watu hasi. Kwa kawaida watu hasi wana kawaida moja kubwa ya kuongea vitu ambavyo havina msaada wa kimaisha kama vile kukatisha tamaa.
Watu wenye mafanikio kwa sababu wanawajua watu hasi jinsi walivyo na hawana mchango wao basi, hujikuta huwakwepa kwa namna fulani watu hawa  hasi na inafika muda kuwapotezea kabisa na kufata maisha yao.
2. Hawapotezi muda wao kufanya kazi bila kuwa na mpango.
Hakuna kitu kibaya kama kuanza asubuhi yako pasipo kuwa na mpango, yaani unamka tu na hujui ni wapi ambako unakoelekea na matokeo yake unajikuta unapoteza muda mwingi huelewi ni kipi cha kufanya.
Watu wenye mafanikio hawafanyi kosa hili hata siku moja. Hawa ni watu wa kuangalia vitu vyao mapema sana na kujua ni kipi kifanyike wapi na lini na wakati upi. Kwa kupangilia kwao huko mambo inawapa nguvu sana ya kufanikiwa.
3. Hawapotezi muda wao kuhofia mambo ambayo hawawezi kuyatawala.
Kuna mambo ambayo hata ukiyahofia vipi huwezi kuyatawala. Dawa ya kusonga mbele na kuachana na mambo haya ni kuyaacha kama yalivyo. Mambo haya yananaweza yakawa kama vile habari na mengineyo kama hayo.
Sasa watu wenye mafanikio ni watu ambao wanapuuza sana mambo kama hayo. Ni watu ambao hawashuguliki kabisa na mambo ambayo wanashindwa kuyatawala. Kila wakati wanahusika na mambo ambayo wanaweza wakayatawala wao wenyewe.
4. Hawapotezi muda wao kuumizwa na mambo  yaliyopita.
Kuna msemo mmoja wa Kiswahili unasema ‘yaliyopita si ndwele na tugange yajayo.’ Watu wenye mafanikio hawapotezi muda kuumizwa na matokeo yaliyopita. Watu hawa kazi yao kubwa ni kufanya yale ya mbele ili kubadili matokeo.
Ili kufikia mafanikio watu walioa na mafanikio wanajua namna ya kucheza na alama za nyakati za kutokuumizwa na mambo ambayo yamepita na mambo ambayo hayana msaada kwao. Kwa kufanya hivyo hupiga hatua sana za kimaisha.
5. Hawapotezi muda kuzingatia sana yale yanayofanywa na watu wengine.
Kuna watu ambao wanaumizwa sana na yale ambayo wanayafanya watu wengine kwenye maisha yao karibu kila siku. Watu hawa badala ya kukazana na juhudi zao wanajikuta ni watu wanaokazana na juhudi za maisha ya watu wengine.
Ili kufanikiwa unatakiwa kuishi maisha yako. Kuendelea kuishi maisha ya watu wengine hiyo inakuwa ni sawa na kuchukua uamuzi wa kujiumiza sana wewe mwenyewe pasipo kujua . chukua uamuzi wa kuishi maisha yako wewe.
Kwa kifupi, hayo ndiyo mambo ambayo watu wenye mafanikio hawapotezi muda wao katika kuyafanya, je, wewe jiulize bado unaendelea kufanya mambo haya.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,









Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel