Wazo La Kujiajiri: Biashara Ya Vikombe Vya Chai Vyenye Kubadili Rangi Vikiwekwa Chai Au Maji Ya Moto.

Wazo la kujiajiri nini? Wazo la kujiajiri  ni wazo ambalo limeanzishwa na uongozi wa mtandao huu wa dira ya mafanikio, lengo ikiwa ni kukupa mawazo mbalimbali ambayo yatakusaidia sana kwa namna moja ama nyingine ili uweze kujiajiri.
Tumeamua kufanya hivyo kwa sababu kuu mbili ambazo ni; mosi tumegundua kwamba watu wetu wengi wanazo pesa ila hawajui namna kuwekeza pesa hizo katika kufanikisha kujiajiri kupitia pesa hizo.
Pili, tumeamua kufanya hivyo kwa sababu kuna baadhi ya watu wanatamani  sana kufanya biashara fulani ila hawajui waanzie wapi, kwa maana ya kupata bidhaa husika. Sisi kama kama Dira tutakupa mawazo mbalimbali na kama utakuwa tayari utawasiliana nasi, tutahakikisha kile ambacho unatamani kufanya kupitia wazo ulilosoma hapa unakifanikisha.

Baada ya kusema hayo machache kuhusu wazo la kujiajiri sasa naomba twende moja kwa moja  kwenye wazo letu la kujajiri ambalo ni wazo  biashara ya vikombe vya chai vyenye uwezo wa kubadili rangi yake kwenda kwenye rangi nyingine mara kikombe hicho kinapowekwa chai au maji ya moto.
Naam, wala usishangae najua tumezoea kunywa chai kwa kutumia vikombe hivi vya kawaida ambavyo havina kitu cha kushangaza pindi utuamiapo. Sasa katika wazo letu la kujiajiri tunakuleta wazo jipya ambalo kwa baadhi ya watu huenda likawa ni geni kabisa. Wazo hili si jingine bali ni vikombe vya udongo ambavyo hubadili mwonekano hasa pale vinapowekwa maji ya moto au chai.
Vikombe hivi ni vizuri sana ndugu yangu kwa sababu ya uimara wake lakini najua pindi utakapoamua kuifanya biashara ya vikombe hivi utawashangaza wengi sana na kiukweli utapata wateja wengi sana. Chukua sekunde chache wawaze mamantile waliopo mtaani kwako, usiishie hapo endelea kuwaza mahotel ambayo upo nayo karibu.
Endelea kuwaza wale watoto ambao hawapendi kunywa chai, vipi ukimpa mtoto huyo chai kwenye kikombe ambacho kitaonesha sura yake pamoja na jina lake bila shaka mtoto huyo hata kusumbua tena kwenye suala la kunywa chai na uji pia, kwa sababu mtoto huyo atashangaa majabu ya kikombe hicho pia hivyo atakunywa tu.
Endelea kuwaza kwa sauti ya chini, Vipi mumeo anaamka asubuhi kabla ya kwenda kazini anakuta umemuwekea maziwa kwenye kikombe kimeandikwa “ I love you Benson” na hilo ndilo jina la mumeo na akimaliza kunywa chai hiyo hayo maandishi yanatopea hadi kesho tena kikombe hicho kikiwekewa chai, bila shaka mumeo huyo atafarijika na michepuko haitakuwa  nafasi tena na utafurahia ndoa yako.
Kwa mifano hiyo michache utaona ni kwa namna gani vikombe hivo jinsi vitakavyokupa hela nyingi kwa sababu kwa hapa nchini kwetu havipo kwa wingi, hivyo bado ni fursa ambayo ni mbichi kabisa. Hivyo ni nafasi yako mwafaka wa kukamatia fursa hii na kuanza kuifanyia kazi ili uanze pia kujitengenezea pesa.
Kumbuka; Vikombe hivi  hubadilisha rangi, picha, maneno  kila vinapowekwa chai au maji ya moto hivyo ni fursa sana kama utaifikiria  kwa jicho la tatu.
-------------------------------------------------------------------------------------------------
MUHIMU: Kama utakuwa  upo tayari na unahitaji kufanya biashara hii wasiliana na uongozi wa kwa nambari 0757 909 942 au bofya namba hii tuwasiliane kupigia whatsapp wa.me/+255757909942  hii au email yetu ya dirayamafanikio@gmail.com
------------------------------------------------------------------------------------------------
Makala hii  imeandikwa; Benson Chonya
------------------------------------------------------------------------------------------------

Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel