Mambo Muhimu Mnapaswa Kuelewa Wakati Mnapitia Nyakati Ngumu Kiuchumi Kwenye Mahusiano Ya Ndoa.

Kuna wakati katika  maisha ya mahusiano yako ya ndoa unaweza usiyaelewe kabisa, hii ni kwa sababu kuna wakati mnaweza mkajikuta katika maisha hayo ya ndoa mnakata tamaa kabisa ya kuendelea kuishi pamoja, hii ni kwa sababu ya ugumu wa maisha ambao mnaupitia.
Tumekuwa mashuhuda wazuri sana kwa kuona ndoa nyingi zikivunjika katika karne hii,  hii ni kwa sababu ya ugumu wa kiuchumi ambao umejitokeza katikati ya safari ya mahusiano hayo ya ndoa.
Zipo sababu nyingi ambazo husababisha mahusiano mengi ya ndoa kufa  ila kubwa zaidi ni suala la kuyumba kwa kiuchumi baina ya wanandoa hao husasani ukosefu wa kifedha katika kutekeleza mambo mbalimbali.
Wapo  pia baadhi wa wanawake wamediriki hata kunyanyua vinywa vyao kuwatamkia waume zao kuwaita wanaume suluari hii yote ikiwa waumeo hao wameyumba kiuchumi hawawapi mahitaji yao ya kifedha kama ilivyokuwa hapo awali.

Kwani hapo awali, mwanzo wa mahusiano hayo walikuwa wanapewa kila kitu kutoka kwa wanaume wao, ila kwa sasa wamekuwa hawapati tena kile walichokuwa wanapewa mwanzo. Ikumbukwe kuwa wanawake hao wamesahau kwamba katika safari  mahusiano ya ndoa kuna kupanda na kushuka.
Kuna wakati mtakuwa katika hali nzuri kiuchumi na kuna wakati mtakuwa na hali mbaya sana kiuchumi. Hivyo mkiona mnapitia wakati mzuri kiuchumi katika mahusiano yenu mnapaswa kumshukuru mwenyezi Mungu.
Pia mnapopitia nyakati ngumu kiuchumi katika mahusiano yenu ya ndoa ni kwamba mnapata kumshukuru Mungu kwa hatua ambayo mnapitia pia, Hii ni kwa sababu wapo baadhi ya watu katika mahusiano ya ndoa wanapopitia kipindi ambacho wameyumba kiuchumi wao hukata tamaa kabisa.
Wengi wao wamefika hatua ya  kutoona thamani ya kuendelea kuishi tena kwa pamoja kwa sababu eti mambo yamekuwa  hayaendi sawa. Ukiona hata wewe umefikia hatua hii kumbuka kwamba mnakaribisha shetani aweze kuyasambaratisha mahusiano yenu.
Kitu pekee ambacho mnapaswa kuelewa wakati mnapitia nyakati ngumu kwenye mahusiano ya ndoa hususani suala la kuyumba kiuchumi mnapaswa kufanya mambo yafuatayo;
Mtangulizeni Mungu;
Kama nilivyosema hapo awali kwamba katika mahusiano ya ndoa kuna kupanda na kushuka, kuna wakati mtakuwa vizuri kiuchumi na kuna wakati pia mtakuwa katika nyakati ngumu.
Hivyo inapotokea  hali kama hii mnapaswa kuelewa Mungu ndiye muweza wa kila jambo, hivyo mnapaswa kumuomba awasaidie kuyalinda mahusiano yenu ya ndoa, vile vile  mnapaswa kumuomba yeye  ili aweze kuwasaidia katika kunyanyuka na kukua kiuchumi.
Msiruhusu Mawazo hasi yawatawale.
Inapotokea mmeyumba kiuchumi hampaswi kuyafanya mawazo hasi yatawale akili zenu, hii ni kwa sababu ninyi ni watoto wema wa Mwenyezi Mungu na mawazo hasi ni ya shetani.
Hivyo mnapoyaruhusu mawazo hasi yatawale akili zetu ni kwamba ninyi mtaona njia bora ya kutatua tatizo hilo ni kuachana na kufanya kila mtu afanye mambo yake, kitendo hicho si kizuri kwa sababu mnakiuka kiapo chenu cha ndoa pia mnamkaribisha shetani aweze kuwatala vyema.
Shirikianeni katika kazi.
Miongoni mwa mambo yatakayowasidia kwa namna moja ama nyingine kuweza kuwa na mahusiano ya ndoa yaliyobora ni pamoja na kushirikiana vyema katika kufanya kazi.
Ni muhimu kushirikiana vyema  katika kufanya kazi kwa sababu hata pale inapotokea kuna anguko la kiuchumi basi wote muweze kujua ni wapi ambapo pamewafanya mpate anguko hilo la kiuchumi.
Jambo hili ni muhimu sana, hii ni kwa sababu ndoa nyingi zinaamini mtu mmoja ndiye ambaye atahusika kuinua uchumi wa familia, hili si kweli bali ukweli mnatakiwa kushirikiana vizuri kwenye kila kazi mnayoifanya ili mjue faida na hasara mnayoipata katika kazi fulani muifanyayo.
Jifunzeni kuweka akiba.
Ili msiweze kupata anguko la kiuchumi kwa namna moja ama nyingine basi kila wanandoa ni vyema wakajifunza kuweka akiba. Kuweka akiba ni muhimu sana kwa sababu kuna wakati akiba hiyo hutumika hasa pale unapokuwa umepatwa na anguko kiuchumi.
Hivyo kivyovyote vile wanandoa mnapaswa kujifunza juu ya utaratibu wa kuwekea akiba ila akiba hiyo iweze kuwasaidia baadae  hasa pale mnapopata angulo la kiuchumi.
Jifunze kutokana na makosa.
Kuanguka kiuchumi isiwe sababu kwa wanandoa kukata tamaa bali liwe na somo kwao kuona ni wapi ambapo wamekosea na kurekebisha makosa yao.
Pia ikumbukwe kuwa unafuu wa kila jambo hususani suala la unguko la kiuchumi kwa wanandoa hutokana na anguko hilo kama somo la kuweze kurekebisha makosa ili baadae waweze kuwa vizuri zaidi.
Hivyo ikiwa mmepata anguko katika mahusiano yenu ya ndoa mnapaswa kujifunza namna ya kutokana na anguko hilo ila baadae msiweze kuanguka tena.
Mkiyazingatia hayo yote ambayo nimeyaeleza kwa siku ya leo ni kwamba maisha yenu ya ndoa yatakuwa ni mzuri sana, kila mmoja wetu atayafurahia mahusiano hayo. Asante.
Ndimi;  Afisa Mipango Benson Chonya
0757-909942




Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel