Vitu Hivi Havifatiliwi Katika Maisha.

Mara nyingi sana, hakuna mtu ambaye anapenda kufatilia vitu vilivyokufa au vitu vilivyokosa matumaini. Kila mtu anapenda kufatilia vitu vilivyo hai, vitu ambavyo vinaweza vikamsaidia leo na kesho pia.

Kwa mfano, kama umelima shamba, na shambani kwako kuna mimea imekufa, mimea hiyo iliyokufa utakuwa huna muda wa kuifatilia kabisa, utachokuwa ukifatilia ni mimea hai na yenye faida kwako.

Na kwenye maisha iko hivyo hivyo. Hakuna mtu ambae yuko tayari kufatilia vitu vilivyokufa. Ukiona watu hawakufatilii sana, basi elewa mambo yako mengi yamekufa na hakuna wa kutaka tena kuyajua.

Kama mambo yako mengi yamekufa, hakuna wa kukufatilia hiyo iko wazi. Kama unataka mambo yako yaanze kufatiliwa hakikisha kila kitu unakifanya kiwe hai. Kila kitu kifufue, utafatiliwa sana na hutaamini.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

 

Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel