Kama Unataka Mafanikio Ishinde Sauti Hii.

Inawezakana umesema unaweza kuishinda changamoto hii iliyo mbele yako, lakini ndani yako bado kuna sauti inayokwambia kwamba hiyo changamoto huwezi kuishinda. 

Inawezekana umefanikiwa kuushawishi ulimwengu wa nje kwa hicho unachokifanya, lakini umeshindwa kuishawishi sauti ya ndani mwako na inazidi kukwambia kwamba huwezi.

Ili kuwa mshindi wa kweli, unatakiwa kuishinda sauti ya ndani yako, sauti inayosema huwezi na kujiambia kwamba sasa unaweza,..unaweza kufanikiwa na kufika mbali kimafanikio.

Kila mtu ndani yake ana sauti hii ya mashaka. Sauti hii haitakiwi kukushinda unatakiwa uishinde na ujiambie unaweza, unaweza. Kila siku sema naweza, naweza na utashangaa utaweza kweli.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

 

 

Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel