Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuachana Na Tabia Ya Kujihukumu.

Kuna wakati katika maisha yako unaweza ukajiona umekosea hili ama lile na lile na kuhisi umeharibu maisha yako kabisa. Kukosea kwa mambo hayo ambayo unaona kabisa ulitakiwa kuyafanya kiusahihi lakini yamekuwa sivyo ndivyo, hali hii hupelekea kuumia moyo na kujihukumu kila wakati.
Ni hali ambayo huwa inatukuta wengi wetu nakujiona ni wakosefu kutokana na kuhukumiwa huko. Hali hii inapotokea kwa muda huwa siyo tatizo kubwa sana lakini inapozidi hapa ndipo ambapo inakulazimu kutafuta tiba ya kukutoa huko kwenye kujihukumu.
Inawezekana ukawa ni miongoni mwa watu ambao huwa wanajihukumu sana ama ulishaona watu wako wakaribu wakiwa hivyo. Kama ni hivyo unatakiwa kuchukua hatua zitakazo kufanya uachane na kujihukumu huko ambako kunakupotezea furaha.
Fuatana nasi katika makala hii kujua hatua muhimu unazotakiwa kuchukua ili kuachana na tabia ya kujihukumu:-
1. Acha kujilinganisha na wengine.
Kama una tabia ya kujilinganisha na wengine sana ni lazima utakuwa mtu wa kujihukumu ndani yako iwe kwa vibaya au vizuri. Ikiwa itatokea wale unaojilingisha nao wakawa wamekuzidi kimaisha kwa sehemu kubwa ni lazima utajihukumu vibaya na kujiona wewe pengine hufai na si chochote katika maisha yako.
Watu wengi ambao huwa wanatabia hii ya kujilinganisha na wengine, ni watu ambao huwa wanajihukumu sana tena kwa vibaya. Kwa kadri wanavyozidi kujihukumu badala ya kuboresha maisha yao ndivyo hujikuta wanaya bomoa zaidi. Na hiyo huwa inatokea kwa sababu huwa wanashindwa kuchukua hatua na kubaki kujihukumu.
Ili uweze kutoka hapo na kuweza kuishi maisha ya furaha na yasiyo ya majuto unalazimika wewe binafsi kuachana na tabia ya kutokujihukumu tena. Unatakiwa kuishi wewe kama wewe kwa kukimbia mbio zako mwenyewe na siyo kuiga maisha ya watu ambayo yanaweza yakakuumiza na kukutesa siku zote.

2. Jiamini wewe kama wewe ulivyo.
Unapokuwa unajiamini wewe binafsi kuwa unaweza inakuwa siyo rahisi sana kwako kuweza kujihukumu bila sababu. Ni lazima utambue kuwa una uwezo mkubwa ndani yako usioweza kuzuiliwa na kitu chochote. Hivyo, ni muhimu kuutumia uwezo huo ulionao ndani yako kuweza kukufanikisha.
Jifunze kuchukua hatua mathubuti ambazo zitakupelekea wewe uweze kujiamini. Kama kuna kitu huna iwe maarifa au chochote kile weka utaratibu wa kujifunza au kupata kitu hicho. Kwa kuwa na maarifa hayo hiyo itakuwa ni chachu kwako mojawapo ya kuweza kukufanya ujiamini na hutoweza tena kujihukumu ndani yako.
Ukijaribu kuchunguza kidogo, utaelewa kwamba watu wengi ambao huwa hawajimini mara nyingi ni watu ambao ni wa kujihukumu sana kwa mabaya na kutilia shaka uwezo wao mkubwa walionao. Ili uweze kuachana na kujihukumu nguzo mojawapo muhimu kwako ni kujiamini.
3. Chukua hatua.
Badala ya kukaa na kuzidi kujihukumu chukua hatua za kuweza kukutoa hapo ulipo. Unaweza ukachukua hatua za kuachana na maneno ya wanaokuona huwezi, umeshindwa na pengine hutafanikiwa, hayo yote yanayokufanya uanze kujihukumu. Kama utaendelea kujihukumu tu, itakuwa ni ngumu sana kwako kuweza kufanikiwa.
Kwa kufuata hatua hizo tatu muhimu yaani kujiamini, kuacha kujilinganisha na wengine na kuchuua hatua ni njia muhimu sana ya kukusaidia kuondokana na kujihukumu.
Kwa makala nyingine nzuri zaidi endelea kutembelea kwa kujifunza kila siku na kuboresha maisha yako.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI NGWANGWALU,
0713 048 035,

Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel