Zingatia Jambo Hili Sana, Litakusaidia Kufanikiwa.
Inapotokea kuna kitu hukijui, kuwa mtu wa shukrani, kwa sababu umepata fursa nzuri ya kujifunza juu ya kitu hicho.
Inapotokea unapitia magumu katika maisha yako, shukuru pia, kwani magumu hayo yanakufanya uwe bora na imara.
Ikiwa pia unapitia changamoto sana, huo sio wakati wa kukimbia, bali ni wakati wako wa kujiboresha kimaisha.
Unapokuwa umechoka kwa sababu ya kazi, basi pia huo ni muda wa kushukuru, kwa sababu kuna mabadiliko umefanya.
Kama umefanya makosa, pia shukuru, kwa sababu hiyo inakukumbusha ni kipi ambacho hutakiwi tena kukifanya.
Ni rahisi sana kuwa na shukrani na mambo mazuri, lakini pia jifunze kuwa na shukrani hata kwenye changamoto.
Watu wengi si wepesi sana wa kushukuru pale wanapokutana na magumu. Ni watu ambao wanakuwa hawaoni zuri lolote.
Kipo kitu chanya au kizuri unaweza kukiona pia kwenye changamoto. Usilalamike, jifunze kupitia changamoto yako.
Yapo mafanikio na baraka ambazo zimejificha kwenye changamoto. Unatakiwa uyaone mafanikio hayo.
Changamoto unazopitia zina uwezo wa kukufanya, ujifunze, ukue na kuwa jasiri wa kufikia mafanikio yako.
Zingatia, mafanikio yako utaendelea kuyapata kama utakuwa mtu wa shukrani katika kila eneo la maisha yako.
Kuwa na shukrani ni msingi mkubwa sana wa mafanikio yako. Anza leo kuwa mtu wa shukrani, utafanikiwa.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.