Watu Wengi Wanashindwa Kwa Sababu Ya Kitu Hiki...
Je! Unajua kwanini watu wengi hushindwa kufikia malengo yao waliojiwekea kwenye maisha?
Wanashindwa kufanikiwa kwa sababu ni watu wakutaka mabadiliko yatokee mara moja.
Ni watu wanaotaka, matokeo ya haraka, mambo ya kusubiri hayapo kwao na hawataki kusikia.
Hawa ndio watu ambao wanataka biashara yao itengeneze faida ya 1,000,000/= ndani ya wiki mbili za kwanza.
Ni watu ambao hawataki kuiona hasara ikitokea kwao. Watu hawa wamejiwekea malengo makubwa sana,
Hadithi za mfumo wa maisha ya watu huwa zinaanza hivi...
Kwanza, wanaanza kuchukua hatua kubwa. Hawataki kuchukua hatua ndogo zinawachelewesha.
Pili, hujionyesha kwa watu kwamba wamechukua hatua kubwa. Karibu kila mtu ataambiwa kile wanachokifanya.
Tatu, hufanya kazi na labda hata wanaanza kupata matokeo na hapa hufurahia sana kwa matokeo hayo.
Na wanapoanza kupata matokeo mazuri, hapo ndipo mambo yanapoanza kusambaratika au kuharibika.
Ghafla, juhudi waliyokuwa nayo mwanzoni inatoweka, na wanajaa kiburi cha mafanikio madogo.
Utakuta starehe zinaanza.
Wasichana wazuri wao.
Ufujaji wa pesa wao.
Anguko lao linaanza kutokea.
Wanajikuta, tayari wameshindwa, hawana mafanikio tena.
Hapa wanaanza kulaumu wengine kwa kushindwa kwao.
Na mwishowe ...
Wanakata tamaa.
Na kuishia kuacha kabisa hicho walichokuwa wakikifanya.
Sasa unaweza kujiuliza ...
Ikiwa walikuwa na ari na walikuwa na malengo makubwa ...
Ni nini kilichowafanya washindwe?
Jibu ni jepesi tu, watu hawa hawakuzingatia kuchukua hatua ndogo na kwa mfululizo utakaowapa uzoefu, waliwaza makubwa tu.
Usije ukanielewa vibaya, si maanishi usiwe na malengo makubwa. Malengo makubwa kuwa nayo ila hatua ndogo ni muhimu pia.
Huwezi kufika popote kama una malengo makubwa na kusahau, kuchukua hatua ndogo ndogo.
Utafika popote kimaisha, kama utazingatia kuchukua hatua ndogo ndogo na kwa mfululizo.
Kila siku fanya mabadiliko madogo na maboresho ya maisha yako na isije ikatokea umeacha.
Watu wengi wanashindwa kwa sababu ya kutaka mabadiliko ya mara moja na makubwa. Hawataki mabadiliko madogo.
Ili kuwa mshindi wewe kila siku,..
Tafuta ushindi mdogo.
Na mwishowe ...
Utafika pale ambapo kila wakati ulitaka kufika.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.