Njia Mbili Ziletazo Mafanikio Maishani.

 

Katika kufikia mafanikio yoyote yale, huwa zipo njia za kuweza kufikia mafanikio hayo. Hakuna mafanikio ambayo yanapatikana nje ya njia husika za mafanikio.

Na kwa kawaida, zipo njia mbili bora za kuufikia mafanikio. Hizi ni njia halali ambazo zinatumiwa na watu wote wenye mafanikio ya kweli na halali duniani.

Njia ya kwanza; Njia ya kawaida.

Hii ni njia ambayo mtu anafikia mafanikio makubwa kutokana na malengo anayoyafatilia kila siku. Hapa lazima uwe na malengo ya kuyafatilia kila siku.

Katika njia hii unakuwa na malengo yako, lakini wakati huo huo unakuwa unaenda nayo mdogo mdogo hadi kuweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Hii ni njia bora, inayoaminika, kwa sababu kuna kujifunza mengi ndani yake, ingawa inataka muda na uvumilivu, lakini mwisho wa siku utafika.

Njia ya pili; Njia isiyo ya kawaida.

Hii ni njia isiyo ya kawaida kwa sababu ndani yake kuna kuwa na hali hatarishi nyingi. Kwa mfano, kuna kuweka mtaji mkubwa ndani yake au kuchukua hatua kubwa kabisa.

Katika kutekeleza njia hii iko hivi, unakuwa unafata njia ile ya kawaida kama kawaida, isipokuwa katika njia hii kuna vitu ambavyo vinaongezeka.

Katika njia hii lazima utenge kiasi fulani cha pesa, ili kuingiza katika 'dili' ambazo zinajitokeza kati kati lakini wakati huo ukiendelea na njia ya kwanza.

Kufata njia ya pili hatumaanishi njia ya kwanza umeiacha, hapana unakuwa nayo,  isipokuwa hii unaitumia kama ziada kutengenezea pesa ndefu.

Hizi ndio njia kubwa mbili, ambazo zinatumiwa na watu wengi wenye mafanikio kuweza kufanikiwa. Ni muhimu kutumia njia zote mbili ili kujihakikishia mafanikio.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

 

Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel