Jinsi Ya Kupika Tambi Za Mayai.
Wednesday, October 13, 2021
Najua kila wakati tumekuwa tukikuletea makala mbalimbali ambazo kimsingi zimekuwa zikikusaidia kwa namna moja ama nyingine katika kuulisha ubongo chakula ya akili. Au kwa maneno mengine elimu ambayo umekuwa ukiipata hapa imekuwa ikikusaidia kuzaliwa upya kifikra hatimaye kutimiza kusudio lako hapa duniani.
Lakini katika makala ya leo nataka tujikite katika masuala mazima ya mapishi. Najua utakuwa unashangaa vipi leo afisa mipango kuleta somo hili. Wala usishangae kila kitu ambacho unakiona katika dunia hii ni fursa. Inawezekana kabisa ukawa hauna lengo la kupika aina hii cha chakula.
Ila kutokana na ulichojifunza hapa kukusaidia kutoa elimu kwa watu wengine na wao wakalipa pesa au chakula hiki unaweza ukakipika katika sehemu mbalimbali kama katika sherehe mbalimbali na wageni waalikwa na wasio waalikwa wakafurahia aina hii cha chakula.
Au unaweza ukapika aina hii ya chakula kwa ajili ya biashara kama vile kwenye mahoteli, migahawa na sehemu nyinginezo.
Hebu tuangalie mahitaji kwa ajili ya kupika aina hii cha chakula.
1. Tambi 1/2 paket
2. Vitunguu maji 2 vikubwa
Karoti 1
3. Vitunguu swaumu kijiko 1 cha chakula
4. Carry powder kijiko 1 cha chai
pilipili hoho 1
5. Njegere zilizo chemshwa 1/2 kikombe
6. Mafuta ya kupikia kiasi
7. Chumvi kwa ladha upendayo
MAANDALIZI YA CHAKULA HIKI
a) Chemsha maji yachemke haswaa, tia chumvi na mafuta kiasi, weka tambi katika maji yaliyo chemka ziache ziive kiasi; kisha chuja maji na uziache kavu.
b) Chukua bakuli pasua mayai kisha weka pembeni.
c) Chukua kikaango kilicho safi weka jikoni tia mafuta kiasi na utaendelelea kuweka vitunguu maji,vitunguu swaumu,hoho ,karoti na carry powder,kaanga kwa pamoja katika moto mdogo mdogo na havitakiwi kuiva sana.
d) Kisha tia tambi na njegere katika mchanganyiko wako na uendelee kukaanga kwa dakika kadhaa.
e) Chukua mayai tia katika tambi ongeza moto kiasi, ili tambi zako zichambuke ,moto hautakiwi kuwa mdogo sana ikiwa moto ni mdogo tambi zako zitashikana na kutia mabonge , mayai ya kiiva hapo chakula chako kitakuwa tayari kwa kuliwa.
Mpaka kufikia hapa chakula chako kitakuwa tayari kwa ajili ya kuliwa, chakula hiki wakati wa kula unaweza ukawa unashushia na juisi ambayo unayopendelea kunywa.
"Mwili hujengwi kwa mawe bali hujengwa kwa kula"
Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya.