Chagua Mwendo Upi Unakusaidia Kufanikiwa.
Kuna wakati unaweza ukakamilisha mambo mengi sana, kama utaamua kwenda kwa taratibu. Unatakiwa usikimbize mambo yako, ila unatakiwa kwenda taratibu na kufanya kwa uhakika na ufanisi mkubwa wenye faida.
Kwa mfano, kama kuna majukumu ambayo unayafanya kila siku, basi, majukumu hayo yafanye kwa utaratibu, kwa utulivu mkubwa na utajikuta unakamilisha mambo mengi ambayo hukutegemea.
Kuna watu wanafikiri ili kukamilisha mambo mengi unatakiwa kwenda kwa haraka zaidi, kitu ambacho si kweli. Unaweza kwenda taratibu na ukakamilisha mambo mengi, unaweza kwenda haraka halafu ukaharibu.
Ni wajibu wako unatakiwa ujue ni wakati upi unatakiwa uende taratibu na wakati upi unatakiwa uende haraka. Si kila wakati wa kwenda kwa haraka ikiwa utafanya hivyo huwezi kukamilisha mambo mengi zaidi unajiharibia wewe.
Kama nilivyosema, kwenda haraka hakuwezi kukusaidia kukamilisha mambo mengi kwa sababu, akili yako inakuwa haijatulia yaani inayumba yumba. Kama akili yako inayumba hivyo, kufanikisha mambo mengi ni ndoto.
Unatakiwa kila wakati kujiuliza, hapo ulipo ni wakati wa kwenda haraka au wakati wa kwenda kwa kasi. Kisha ukishapata majibu, fanya uamuzi sahihi. Maisha sio mashindano na wengine, angalia mwendo wako.
Hapa ndio upo ule umuhimu wa kuchagua mwendo upi unakusaidia kukamilisha mambo mengi. Je, mwendo wa kasi au mwendo wa taratibu, lakini kaa ukijua kila mwendo una sehemu yake.
Suala hili, lipo kama vile unavyoendesha gari. Si kila wakati unatakiwa kukimbiza gari, yapo mazingira yake. Na kwenye maisha iko hivyo hivyo, kuna wakati wa kwenda kwa haraka na wakati wa kwenda taratibu.
Kufanikiwa kwako kunategemea sana uchaguzi wako wa mwendo upi uutumie na katika eneo lipi. Fanyia kazi hili, na utaona matokeo makubwa kwa upande wako.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.