Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Unapotaka Kufanya Uwekezaji.
Ipo hivi unapofanya uwekezaji katika jambo lolote unatakiwa kuelewa kwamba hakuna faida utakayoipata papo hapo. Bali uwekezaji huchukua muda fulani mpaka uje uone uwekezaji wa jambo hilo.
Wengi wanapoambia wawekeze katika jambo fulani hukurupuka katika kuwekeza mwisho wa siku hujikuta wanapata hasara au kutokuona faida ya uwekezaji waliofanya.
Kitu pekee ninachopaswa kukumbusha ni kwamba unapotaka kuwekeza katika jambo fulani, unatakiwa kuzingatia mambo haya machache;
· Uwekezaji unakutaka uweze kulielewa jambo unalotaka kuliwekeza kwa undani zaidi.
· Faida ya uwekezaji huchelewa sana kuonekana.
· Uwekezaji huitaji uvumilivu mkubwa ndani yake.
· Uwekezaji unahitaji umakini wa hali ya juu ili kuepukana kupata hasara ya jambo husika.
Hivyo ni vyema ukayazingatia hayo machache kati ya mengi kabla hujaamua kuwekeza katika jambo lolote lile ulitakalo.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Ndimi: Afisa Mipango Benson Chonya.
0757-909942