Sababu Nne (4) Kwa Nini Maisha Yanazidi Kuwa Magumu Kwa Wengine.

Kwa miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na wimbi kubwa la watu linalalamika kwamba maisha yamekewa magumu. Kwa sababu hii pia watu wengi wamekuwa wakikata tamaa na kuona maisha hayafai ni bora waishi hivyo hivyo ilimradi siku ziende.
Malalamiko ya maisha kuzidi kuwa magumu yamekuwa yakisikika sana karibu ulimwenguni kote. Na kwa hili  hiyo imekuwa ikipunguza raha ya kuona ‘utamu’ wa maisha halisi. Si vijana wala wazee kila mtu amekuwa akisema lake juu ya ugumu wa maisha.
Lakini pamoja na malalamiko hayo, kitu ambacho tunatakiwa tujiulize nini kinachopelekea kuwe na ugumu wa maisha kila kukicha? Makala haya ya leo inakwenda kukupa majibu kwa nini  maisha yanakuwa magumu kwa wengi zaidi.

1. Kutegemea chanzo kimoja cha mapato.
Kutokana na maisha kubadilika na gharama za maisha kupanda karibu kila siku, suala la kutegemea kipato kimoja, ni moja ya chanzo cha maisha kuwa magumu. Watu wengi wanategemea kipato kimoja, zaidi kwa wengi ikiwa ni ajira.
Kwa bahati mbaya kipato kimoja hakiwezi kukidhi mahitaji yote hata iweje. Sasa kwa sababu hiyo ya maisha kupanda mara kwa mara, ni lazima tu ugumu wa maisha uonekane. Hata siku moja usitegemee maisha yako yakawa rahisi kama bado una kipato kimoja.
2. Watu wengi wanafanya vitu wasivyovipenda.
Maisha ni magumu pia kwa watu wengi chini ya jua kwa sababu wamekuwa ni watu ambao kila siku wanafanya kazi ambazo wasizozipenda. Kama unafanya kazi usiyoipenda, unategemea nini, lazima maisha yatakuwa magumu tu.
Kufanya kazi usiyoipenda, kwa kawaida kunakuwa kunakuchosha sana na unakuwa unaifanya tu, kwa sababu eti upate pesa ya kula. Kama umechagua maisha hayo, ujue kabisa maisha hayo yatazidi kukufanya wewe uyaone magumu kila kukicha.
3. Watu wengi wanaishi juu ya matumizi.
Ugumu wa maisha pia kwa namna moja au nyingine unachangizwa na watu kuishi juu ya matumizi au vipato vyao halali. Unatakiwa kuelewa watu wengi, wanaishi juu ya matumizi kwa sababu ni watu ambao wanataka waonekane wamefanikiwa.
Watu hawa wanakuwa wapo tayari wakope au wafanye lolote lile ili waonekane mambo yao yako safi. Kwa msingi huo wanakuwa wanajitengenezea maisha magumu ambayo wanashindwa kuyamudu kwa urahisi na matokeo yake kuongeza ugumu usio na sababu.
4. Hakuna anayejali sana maisha ya wengine.
Maisha ya sasa hivi naweza kusema yamekuwa ni kama ya kuishi kisiwani, watu wamekuwa hawajali sana watu wengine kwa kiasi kikubwa, ukilinganisha na zamani. Kwa sasa ukipata changamoto kubwa wewe jua hiyo ni changamoto yako tu, inabidi ukomae nayo hadi utoke.
Kutokana na hili kuendelea kudumu kunafanya maisha yanazidi kuendelea kuwa magumu sana hadi watu wanakosa msaada ambao ungeweza kuwasaidia. Ubinafsi ambao wengi wanao imekuwa ni kichocheo kikubwa sana cha ugumu wa maisha.
Mwisho, pengine ujiulize, je, maisha yanaendelea kuwa magumu kwako kila kukicha? Jibu unalo wewe, nimekupa walau sababu chache zinazoonyesha kwa nini maisha yanazidi kuwa magumu. Wewe unaamini nini, niwekee maoni hapo chini.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0687449428, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE.






Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel