Nguvu Ya Changamoto.

 

Kuna wakati unajikuta upo kwenye siku ambayo una vitu vingi sana vya kufanya, lakini cha ajabu huwa ni siku ambayo pia unaweza kukamilisha mambo mengi ambayo hukutarajia.

Pia kuna siku ambayo unajikuta una vitu vichache vya kufanya, lakini huwa ni siku ambayo hukamilishi mambo mengi pia. Unashangaa unajikuta, mambo mengi hujafanya.

Hiyo inamaanisha nini, kila unapokuwa kwenye changamoto, akili yako inakuwa na nguvu na uwezo wa kufanya mambo mengi na kufanya kazi vizuri na ufasaha mkubwa. 

Unatakiwa ujue, changamoto unazokutana nazo,  zinakuwa zina uwezo mkubwa wa kuamsha akili yako na kuifanya ifanye kazi kwa njia ya maajabu na kuleta majibu ya kushangaza. 

Hivyo, fundisho kubwa hapa ni kwamba, hutakiwi kuogopa changamoto, kwani changamoto zinakukomaza na kukusaidia kukamilisha mambo mengi. Changamoto ni msaada kwako.

Kila unapokutana na changamoto, jiulize, utawezaje kufanya na kupata majibu sahihi. Hakuna kinachoshindikana kila kitu kinawezekana hata ukiwa kwenye changamoto. 

Ipo nguvu kubwa sana ndani ya changamoto, kama utaelewa vizuri. Yale ambayo ulikuwa huwezi kuyafanya unaweza kuyafanya ukiwa kwenye changamoto kubwa na za kutisha.

Kuanzia leo, acha kuhuzunika unapokutana na changamoto, jifunze juu ya changamoto hizo. Kazi ni kwako, weka akilini changamoto wakati wote ni msaada kwako, zitakuimarisha na kukufanikisha.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel