Sababu Inayokufanya Urudi Nyuma Kimafanikio.
Kuna wakati inatokea mambo yako yanaenda vizuri, ghafla changomoto inatokea na kukurudisha nyuma kabisa.
Je, ulishawahi kujiuliza kwa nini hali hiyo inatokea kwako, na pengine wapi unakosea sana hadi iwe hivyo kwako wewe?
Kwa mfano, utakuta kipato chako kinaanza kukua, ila kuna jambo linajitokeza na unajikuta unatumia pesa zote.
Unakuta ni kweli umeanza mahusiano yako mapya vizuri, lakini ghafla kuna kitu kinaingilia na kuharibu mahusiano hayo.
Unakuta umeanza biashara yako vizuri, lakini ghafla zinatokea changamoto ambazo zinaharibu kabisa biashara hiyo na kuiua.
Unakuwa ni kama mtu ambae unaenda hatua tatu mbele, lakini unarudi hatua tano nyuma. Kitu hiki kinatokea sana kwa wengi.
Kuna wakati unakuwa una waza una mkosi? lakini unachotakiwa kujua upo kwenye changamoto inayosababishwa na wewe.
Hakuna mkosi wala laana uliyonayo, unatakiwa ujichunguze ni wapi unakosea sana hadi iwe hivyo kwako.
Kama usipojipa umakini wa kujichunguza na kuangalia hasa sababu ni nini, basi utaishia kukwama hapo hapo.
Usitafute mchawi, tatizo na chanzo kikubwa ni wewe, angalia ni wapi unakosea na kisha jirekebishe, songa mbele.
Inawezekana unaenda mbele na kurudi nyuma sababu ya tabia zako au mahusiano mabaya na wengine, chunguza, majibu utapata ya kukusaidia.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.