Makosa 28 Ambayo Hutakiwi Kufanya Kwenye Maisha.
Yapo makosa ambayo pengine kwa kutokujua, uliyafanya na yamekufanya unashindwa kufikia viwango vile vikubwa vya mafanikio ulivyokusudia.
Na makosa hayo hutaki yajirudie kwako, na hutaki mwingine akutane nayo. Katika makala hii inakuonyesha makosa hayo kwa wazi.
1. Kutokuthubutu, wakati una uwezo wa kuthubutu kufanya hicho unachotakiwa kukifanya na kikakupa mafanikio makubwa.
2. Kutokujifunza elimu sahihi ya fedha na mafanikio mapema, ni kosa ambalo ukilifanya utalijutia sana maishani baadae.
3. Kufanya biashara ambayo una hadithiwa inalipa na wakati wewe huijui na hujawahi kuifanya na unaingiza pesa za kutosha.
4. Kuharibu mahusiano ya watu, eidha yawe ya kibiashara au kimapenzi.
5. Kuwa na marafiki ambao sio SAHIHI kwenye maisha yako.
6. Kufanya maamuzi yasiyo sahihi kabla hujafikiria vya kutosha.
7. Kuwaamini watu ambao hukustahili kuwaamini na ukaamua kuwaelezea kila kitu. Kujiachia sana kwa watu sio kuzuri.
8. Kutokujua kwamba mtaji si pesa tu, hata uaminifu nao ni mtaji mzuri sana, kama ukiutumia kwa uaminifu na uhakika mkubwa.
9. Kuacha ulichokuwa ukikifanya, na kuamua kukimbilia kwenye kitu kingine kipya. Huko ni kupoteza nguvu bure, ulichokuwa ukikifanya, hakitafanikiwa na hicho kipya hakitafanikiwa pia.
10. Kuanzisha biashara mpya na kuacha watu wasimamie na wewe ukiwa mbali, ni kosa kubwa sana kibiashara.
11. Kuanzisha mahusiano na mtu usiyemjua vizuri, halafu mwisho wa siku yule mtu anakuja kukupotezea muda na pesa zako bure.
12. Kutumia pesa hovyo na kujikuta ukiwa kwenye madeni makubwa sana.
13. Kughairisha mambo kila wakati kwa kuamini muda upo, kumbe muda haupo.
14. Kumwamini mtu kirahisi rahisi tu ambae humjui iwe kwa kuwasiliana nae au kuishi nae kwa ukaribu.
15. Kuitumia pesa hovyo bila ya kuifanyia mpangilio maalumu. Kabla pesa yoyote haijatumika, ni lazima ipangiliwe na kuwekewa bajeti.
16. Kuamini hutoweza kitu bila kuwa na 'connection' au mtu kati. Unaweza ukaweza hata kama huna mtu mwingine.
17. Kuogopa kuanza upya, mara baada ya kila kitu kuwa kimekwenda hivyo.
18. Kutokuanza na kidogo ulichonacho kwenye maisha yako.
19. Kuchanganya ujasiriamali mchanga na anasa.
20. Kutokuwa mtu wa kutafuta maarifa, unafanya kazi kubwa, lakini unakosea padogo tu, maarifa huna.
21. Kununua vitu bila mpangilio na matokeo yake kuviona tena havikufai vitu hivyo.
22. Kufanya vitu vingi kwa mara moja na kukosa usimamizi.
23. Kutokujikubali kuwa unaweza, na kumbe uwezo wa kuweza unao tu na tena mkubwa.
24. Kuogopa kufanya kitu kwa sababu ya kuogopa kukataliwa au kukosea.
25. Kutokusema hapana, ni kitu kidogo lakini kinakupotezea sana.
26. Kuacha kufanya unachokipenda na kufanya mambo mengine eti ili kuwaridhisha watu.
27. Kuoa au kuolewa na mtu asiye na hofu ya Mungu. Kila ukimwambia hiki, ni mbishi hatari.
28. Kuanza na biashara na kitu kikubwa sana, wakati kwenye biashara kuna kujifunza mengi na kukosea ni lazima.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.