Mambo Matatu Ya Kuifanya Siku Yako Iwe Bora.

Kwa kawaida kuna mambo matatu, ambayo ukiyazingatia, yana uwezo mkubwa sana wa kuifanya siku yako ikawa bora na mafanikio makubwa.

Haya ndio mambo ambayo hutakiwi kuyapuuza, unatakiwa kuyachukulia hatua, ili kila siku kwako iwe bora na manufaa makubwa ya kukusaidia kufanikiwa.

Jambo la kwanza, fanya kitu ambacho kina maana kubwa kwako.

Unatakiwa kufanya kitu ambacho kinakusukuma kufanya sio kwa sababu tu utapata fedha, bali kwa sababu kina maana kubwa kwako.  

Unapofanya kitu ambacho kina maana, kaa ukijua utake usitake utajikuta unajituma tu bila hata kupenda na utajikuta ukifanya makubwa sana.

Jambo la pili, zungukwa na watu ambao ni chanya

Kila siku unatakiwa kuzungukwa na watu chanya kuliko wale ambao ni hasi. Watu hawa chanya wanakufanya uone inawezekana na hivyo kukusukuma zaidi.

Unatakiwa kukumbuka watu hasi wanakurudisha nyuma. Kwa kadri unavyowakwepa watu hasi, hiyo itakusaidia sana wewe kuwa na siku yako bora na yenye manufaa makubwa kabisa.

Jambo la tatu, uwe na nguvu.

Hapa unatakiwa uwe na nguvu ya mwili na akili ndio vinakuwezesha wewe kupata chochote unachotaka.

Kama huna nguvu ya akili au ya mwili, kwa wewe kuifanya siku yako kuwa ya maana na yenye ufanisi huo utakuwa ni uongo mkubwa sana.

Hayo ndio mambo ya msingi, ikiwa utayazingatia basi, yatafanya siku yako kuwa bora na ya faida.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

 

Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel