Haya Ndio Mambo Makubwa Mawili Katika Dunia.

Tupo kwenye Dunia Yenye Fursa
 

Kwa sasa tunaishi katika dunia yenye mambo makubwa mawili, fursa za kutosha na habari za kutosha.  Hakuna kipindi katika mentira ya maisha ya binadamu kimewahi kuwa na fursa na habari nyingi kama sasa. 

Jukumu lako kubwa katika kipindi hiki ni kutuliza akili na kuwa na vipaumbele kwenye fursa, lakini pia kuwa na uthibiti wa habari unazozipokea kila siku. Hayo mambo unatakiwa kuwa nayo makini sana.

Kama kila fursa inayojitokeza kwa sasa utataka kuifanya, unajidanganya. Utaambiwa mengi sana kuhusu fursa lakini unatakiwa kuwa na vipaumbele juu ya fursa hizo, maana zipo nyingi za kutosha na huziwezi. 

Kama ni habari, hapo ndio usiseme kila kukicha kuna habari hii au ile. Hakuna uhaba wa maarifa, tunaambiwa kila baada ya miaka mitatu, maarifa yanatoka na kuja mapya mengine kabisa. 

Kwa dunia hii unaweza ukafanya kitu chochote hata kuwe na vizuizi vipi haviwezi kukuzuia maana utaweza kupata njia ya kutoka kwenye hivyo vizuizi na kupata suluhu kamili ni nini. Kipi kinashindikana kwa dunia hii? 

Kwa kifupi, tupo kwenye dunia ya wazi. Tupo kwenye dunia yenye neema na mafuriko ya habari. Udhibiti wa fursa na habari unatakiwa uwepo, vinginevyo huwezi kufanikiwa. Unatakiwa kutumia vizuri fursa na habari.

JAMBO LA KUZINGATIA NAKUFANYA, elewa tupo kwenye dunia ya fursa na habari. Unatakiwa kuwa makini ili usije ukapotezwa. Weka vipaumbele kutumia fursa, na funga masikio kwenye habari mbaya.

 Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel