Kama Unaogopa Kuchukua Hatua Kwa Sababu Hii, Unajichelewesha.

Kama unaogopa kuchukua hatua eti kwa sababu utaaibika, utachekwa au unaogopa kuonekana mjinga, basi wewe ndio utakuwa mjinga kwa kitendo chako cha kutokuchukua hatua za mafanikio yako. 

Kama kweli huchukui hatua kwa sababu ya kuwaangalia watu wanasema au watasema nini, hilo ni kosa kubwa kwako na unajikwamisha kufikia mafanikio yako. Iweje uogope kuchukua hatua kwa sababu ya watu?

Kama upo kwenye jela hiyo, ya kuogopa kuchukua hatua kwa sababu utachekwa au kwa sababu utaonekana mjinga, basi nikwambie maisha yenyewe ndio yatakayo kuaibisha wewe kwa sababu utakuwa huna kitu.

Wale watu wote wanaonekana wajinga, ndio wanaofanikiwa. Wale wote wanaochukua hatua bila kujali watachekwa au wataambiwa nini, hao ndio huwa wanafanikiwa na kufika mbali. Iweje leo hii wewe uone aibu?

Kama bado unaogopa kuchukua hatua kwa sababu hizo za kitoto, nikwambie unajichelewesha na acha woga wa kijinga. Chukua hatua bila kujali watu watasema nini juu yako, chukua hatua bila kujali kama unachekwa.

Narudia tena, maisha yatakuaibisha vibaya sana, kama utakuwa unaogopa kuchekwa eti kwa sababu ya kile unachokifanya. Fanya chochote kile unachotaka bila kuangalia mtu, na UTAFANIKIWA.

 Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

 

Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel