Usichokijua Kuhusu Freemasons.Je Nikweli Wanatoa Kafara?
Monday, April 25, 2022
UTANGULIZI.
Freemason au freemasonry ni moja ya taasisi kubwa sana ambayo imeenea ulimwenguni na inakua kwa kasi sana, Mason kwa asili walikuwa ni mafundi waliokuwa wakijihusisha na kazi za uchongaji wa mawe na hatimaye ujenzi wa majengo makubwa ya makanisa yaani Cathedrals jina mason lina maana ya mafundi ujenzi au waashi na freemason maana yake ni “Wajenzi huria” wengi wa wajenzi hao walikuwa Wakatoliki na walianzia mnamo katika karne ya 17, mpaka wakati wa mabadiliko makubwa ya kimapinduzi huko Uingereza Mason walijulikana kama watu matajiri na wenye uwezo wa hali ya juu na hivyo wakajulikana kama watu wenye mawazo ya juu na wenye uwezo wa kuhakikisha kuwa kuna usawa, amani na kutatua matatizo na maswala yaliyoleta utata katika jamii, mikutano yao ilikuwa ya kijamii kuliko ya kibiashara na kwa mara zaidi ya nne walikutana na walijulikana kama Kusanyiko la wajenzi, waliungana tarehe 24 june 1717 na kuunda chama chenye kuheshimika sana cha wajenzi katika jiji la London na Westminster ambapo baada ya miaka sita wakawa chama chenye kuheshimika sana nchini Uingereza na baraza hili ndio chimbuko la Freemasons ulimwenguni, chama hicho kilichoheshimika cha ulimwengu mzima kiliundwa katika mji wa York mwaka 1725 na baadaye katika kisiwa cha Ireland ndani ya miezi sita na huko Scotland ndani ya 1736 baraza la York lilitambuliwa kisheria kama chama chenye kuheshimika na maarufu katika Karne hiyo.
Kutokana na mpangilio na utaratibu wa wanachama na hekima yao na kuinuka kwao huko uingereza watu hao walionekana kama wa daraja la juu na watu waliofanikiwa sana na kujipatia umaarufu mkubwa na hivyo watu wengi maarufu na wa Nyanja ya juu katika uingereza walijiunga na mason wakazidi kuwa maarufu, swala la dini lilikuwa swala la msingi na la usawa kwa watu wote ili kuendelea kukuza uhuru wa maswala ya kiroho mpaka mnamo karne ya 18 katika jumuiya zote za wanaozungumza kiingereza swala la dini liliachiwa kwa mtu binafsi, Upinzani mkubwa hata hivyo wa chini kwa chini wa freemason ulikuwa dhidi ya Kanisa Katoliki pamoja na kanuni zake na asili ya dini jambo lililodhoofisha utendaji na maendeleo ya kikanisa na swala hili lilipelekea Freemason kutokuruhusiwa kabisa katika inchi zenye ukatoliki mwingi ikiwamo Huispania, ingawa huko Ufaransa kutokana na imani ya Atheist na Uprotestant na mapinduzi ya kifaransa utaratibu huu ulistawi.
Leo hii Freemason wanajitokeza duniani katika sura tofauti tofauti wakiwa na wanachama wapatao milioni 150,000 chini ya uongozi wa Grand Lodge of Scotland na Grand Lodge of Ireland zaidi ya robo yao wanaongozwa na United Grand Lodge of England na zaidi ya milioni mbili chini ya Marekani yaani United States of America. Maswala ya maongozi wakati mwingine hutolewa kulingana na kila jumuiya inavyoona kulingana na taratibu zao, ingawa vyama hivyo vinatambuana lakini kila jumuiya ina aina zake za maongozi na zinawajibika katika tawi kuu husika la freemason
Freemason hata hivyo wana madai ya kuweko ulimwenguni siku nyingi kihistoria kwani wao hudai wazi kuwa walihusika kulijenga hekalu la mfalme Sulemani huko Israel itakumbukwa kuwa hekalu hilo lilijengwa bila ya mlio wa nyundo kusikika wao walichonga mawe na kisha mawe hayo yalipachikwa na kujenga Hekalu, jamii hii pia inahusika na ujenzi wa miji mingi mikubwa na majengo makubwa kama kumbi za Bunge na Minara katika miji na ubunifu wa maswala mengineyo freemason kusudi lao kuu ni kuuendesha ulimwengu katika njia mpya “New World system” ambapo ulimwengu utaendeshwa kidemokrasia na maswala ya haki za binadamu kuzingatiwa na uhuru wa binadamu kuheshimiwa bila kusumbuliwa au kuingiliwa hii ndio taratibu mpya itakayoongoza ulimwengu katika mpango wa chama hiki cha siri chenye utata mkubwa duniani Fuatana nami basi tunapoendelea kuichambua freemason.
Nimeweka video hapo chini ili uweze jifunza zaidi.
USIACHE KU SUBSCRIBE YOUTUBE CHANNEL YETU NA KUBONYEZA ALAMA YA KENGERE
WAKO KATIKA MAFANIKIO
IMANI NGWANGWALU