Epuka Tabia Ya Aina Hii Katika Safari Yako Ya Mafanikio.

Watu wengi wanashindwa kufanya vizuri katika maeneo wanayoyafanyiaka kazi kwa sababu ya kukosa kwao uwezo wa kujiamini kwenye yale wanayoyafanya. Wao wamekubwa na tatizo kubwa la kujilinganisha  uwezo wao kwenye yale wanayoyafanya na  watu wengine wanaofanya mambo kama yale wanayofanya wao.
Kwa kitendo hiki kimesababisha watu hao kujiona kama vile hawajui sana wakijilinganisha na watu wengine.  Pia kitendo cha kujilinganisha na wengine kimesabasha watu wengine wajione hawana thamani na uwezo wa kufanya vizuri zaidi.
Kwa muktadha huo, unachopaswa kuelewa ni kwamba wakati mwenyezi Mungu alipomuumba mwanadamu alimpa kila mtu uwezo wake binafsi uwezo ambao huwa haufanani na mtu mwingine, kama ndivyo hivyo kwanini uendelee kujilinganisha na wengine.

Tambua kitendo ambacho unakifanya cha kujilinganisha wewe na watu wengine  ni kinyume na sheria za mafanikio pia kitakufanya ujione kama vile hujui na wakati mwingine kitakuondelea kabisa uwezo wako wa kujiamini kwenye kila eneo unalofanyia kazi au unalotaka kufanyia kazi.
Hivyo ukiwa unataka kufanikiwa katika eneo fulani ambalo unalifanyia kazi basi, unatakiwa uache mara moja tabia yako ya kujilinganisha na wengine kwa sababu unajiua wewe mwenyewe pasipo kujua. Unatakiwa kuelewa uwezo wako wa kufanya jambo fulani ni mkubwa sana zaidi ya unavyofikiria.
Na ndiyo maana upo usemi mmoja unasema “Samaki hawezi kupanda juu ya mti, ngedere hawezi kukimbia kama farasi, baadhi ya ndege pori hawewezi kuogelea. Hii ikiwa na maana kila mmoja ana uwezo wake wa kufanya vizuri zaidi kutokana na mazingira ambayo ameyazoea, hivyo ukimwambia samaki apande juu ya mti utaishia tu kumlaumu kwamba ni mjinga, lakini ukweli ulio wazi kwamba siyo mjinga bali siyo sehemu yake sahihihi aliyeizoea.
Samaki uwezo wake mkubwa upo kwenye maji hii kutokana na uwezo wake aliyeoumbwa nao wa kufanyia kazi na kufurahia maisha yake katika maji. Hivyo  hata wewe furahia uwezo ulio nao acha kujilinganisha na wengine kwa sababu kila mmoja ana uwezo wake wa kufanya jambo fulani kutokana na mazingira aliyeyazoea.
Kumbuka unapojilinganisha uwezo wako na mtu mwingine unafanya makosa makubwa sana kwa sababu kila mmoja wetu ameubwa na uwezo wake.
Imeandikwa na Afisa Mipango: Benson Chonya.
0757-909942

Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel