Njia Nne Za Kukabiliana Na Kukosolewa Katika Maisha.
Sunday, April 24, 2022
Katika dunia hii yapo mambo ambayo unaweza kuyakwepa, ila linapokuja suala la kukosolewa na watu wengine kwenye kile unachokifanya au unachotaka kufanya huwa hakuepukiki na huwezi kukwepa, lazima ukosolewe.
Maisha ndivyo yalivyo, kwa vyovyote vile ni lazima watu wakukosoe, katika kukosoa huko kupo kutakokujenga na kupo ambako kutakufanya upoteze mwelekeo kabisa kwenye kitu unachokifanya au unachotaka kufanya, hii inategemea na wewe.
Kama nilivyosema hapo awali kwamba kukosolewa kupo, kila mtu anakabiliwa na kukosolewa. Kukosolewa hakukwepeki katika maisha na ndio ukweli ulivyo. Kama hutaki kukoselewa, basi usifanye kitu, na usiseme kitu chochote.
Haijalishi umekosolewa mara ngapi, haijalishi umekosolewa kwa miaka mingapi, unatakiwa ujifunze kutawala kukosolewa huko. Hivyo, katika makala haya ya leo nitaeleza kwa kina njia nne za kukabiliana na kukoselewa.
1. Potezea kukosolewa kwa njia hasi.
Kila mmoja wetu ana malengo yake ambayo amepanga kuyatimiza baada ya muda fulani, hivyo linapokuja suala la kukoselewa husasani suala la watu wengine kukukatisha tamaa wewe endelea kupambana kwa sababau hayo ni maoni yao hasi.
Kwa mfano unaweza ukawasikia watu wakikukosoa kwamba huwezi kufanikiwa kwenye jambo unalolifanya huenda ikawa ni katika mahusiano, biashara, elimu na mambo mengine kama hayo, wewe puuza hiyo habari.
Kumbuka hayo ni maoni yao binafsi na hakuna wakuyazuia, ila unachotakiwa ni kujifunza kupokea maoni hayo kwa njia hasi, kwa sababu kama utapokea kwa njia ya kauamini kuwa huwezi kufanikiwa katika jambo fulani ni kweli hautaweza.
2. Thamini unapokoselewa kwa njia ya kujengwa.
Kama nilivyosema hapo awali kwamba kuna faida mbili za kukoselewa ambazo ni kukujenga au kukupotezea mwelekeo. Wakati mwingine siyo kila anayekukosea ana lengo ya kukatisha tamaa bali lengo lake linakuwa ni kukufundisha mambo ya muhimu.
Hivyo wakati mwingine usipuuze watu wengine wanavyokukosoa kwa sababu watu wengine wanakuja kwako kama daraja ambalo litakusaidia wewe kwa namna moja ama nyingine kuweza kufanya vizuri zaidi.
Wao kazi yao kwa ni kuona makosa yako na kukupa elimu ya kuweza kufanya vizuri zaidi ili uweze kuboresha zaidi kile unachofanya. Kwa hiyo thamini sana kukoselea kwa njia chanya kutakujenga na kukusaidia kufanikiwa.
Kumbuka unapokosolewa iwe ni kwenye biashara, mahusiano, clan na mambo mengine, unachopaswa kuelewa ni kwamba si kila anayekokosoa lengo lake huwa ni baya, hapana wakati mwingine watu wanapokukosoa wanakusaidia kuweza kukujenga na kukuimarisha zaidi hivyo usiwapuuze.
3. Chukulia kukosolewa ni sehemu ya maisha.
Naam, wala hujakosea kusoma upo sahihi kabisa, kama nilivyosema hapo awali kwamba kukosolewa kupo na kutaendelea kuwepo na hivyo ndivyo ilivyo kwa sababu maisha yana pande mbili yaani watu kupenda kile wanachokifanya pia wapo baadhi ya watu hawatapenda kile unachokifanya,
Watu wanaokupenda watakukosoa kwenye kile unachofanya ili uweze kufanya vizuri zaidi, ila wale wasiokupenda watakukosoa kwenye kile unachofanya ili usiweze kufanya vizuri. Maneno na mitazamo ya watu ipo, uliikuta na utaicha, hivyo usigope na nani anasema nini juu yako.
Kitu cha muhimu ambacho unapaswa kukizingatia ni kuhakisha watu wote waache waendelea kukukosoa kwa sababu watu hao hawaepukiki, ila kwa upande wako fanya upembuzi kwa kuona nani yupo sahihi kisha uchue maoni ya mtu huyo kwenye kile unachokifanya ili kiweze kufanikiwa. Kumbuka kukosolewa ni sehemu ya maisha.
4. Usifikiri kukosolewa kunakuhusu moja kwa moja.
Kukosolewa katika maisha kupo, ila siyo kila anayekukosoa ana lengo zuri la moja kwa moja na wewe, bali unachopaswa kulewa ni kwamba unatakiwa kuchagua watu wanasema nini kuhusu wewe.
Kama yale wanayokukosoa ni ya kujenga basi hakikisha unayabeba na kuyafanya yakufae maishani kwenye kile unachokifanya au unachotaka kufanya ila kama si ya kukujenga unapaswa kuachana nayo na kuacha maisha yaendelee.
Mpaka kufikia hapo kwa leo sina la ziada, ni imani yangu kubwa kwamba kuna mambo muhimu ya msingi ambayo umejifunza yatakayokusaidia kwa namna moja ama nyingine ya kukabiliana na kukosolewa kwenye mambo unayoyafanya au unayotaka kufanya.
Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.
0757-909942