Huu Ndio Muujiza Mkubwa Wa Kula Vyakula Vinavyoishi.

Wewe kama binadamu anayejitambua na kujipenda, unahitaji kufahamu kuwa wewe ni matokeo ya kile ulacho kila siku. Kwa kufanya mageuzi katika lishe yako, unaweza kabisa kubadili maisha yako kuanzia muonekano, nishati/nguvu ya mwili hadi uchumi.
Wengi wetu tayari tunafahamu juu ya ulaji wa kunenepesha mwili au kupunguza mwili, lakini ni watu wachache sana ambao wanatambua jinsi ya kutumia chakula katika kufungua nguvu ambayo mara nyingi upotea kutokana na kutumika katika kusaga na kulainisha baadhi ya vyakula ambavyo havisagiki haraka mfano nyama.
Mikakati yote ya kukuza uchumi, kuleta utulivu wa akili na mbinu binafsi za ustadi wa maisha hazitakusaidia kama hautakuwa na nguvu na afya ya kufanya yote yale yanayohitajika ili kufikia maisha ya ndoto yako.
Makala hii ni juu ya muujiza wa chakula ambacho umewekwa mwilini mwako. Kwa kujali zaidi kupitia lishe sahihi, unapata uhakika wa kuishi maisha marefu na uwezo wa kufikia ndoto zako za maisha bora.

Kwa kuliacha suala nyeti la chakula na lishe lijiendee vyovyote, ni wazi kwamba ndoto zako nyingi zitavunjikavunjika na kamwe hutaweza kuzitimiza hata siku moja.
Katika nchi ya India ya kale, watu wake waliamini kuwa akili na ubongo imara ni vitu vilivyo na uhusiano wa moja kwa moja na aina ya chakula na lishe ya mtu husika. Vyakula vyepesi na ambavyo siyo vya asili ya nyama kama vile mbogamboga na matunda, walivipendelea zaidi.
Watu hawa wenye asili ya India na Asia, walikuwa wakiamini kuwa kutiririka kwa nguvu binafsi na nishati mwilini ni kitu kilichokwamishwa zaidi na ulaji wa nyama. Utafiti wa kisayansi wa hivi karibuni umedhihirisha kuwa utendaji kazi hafifu wa mtu unahusishwa moja kwa moja na hali yake ya akili na mwili.
Wito kwako msomaji wa ni kwamba ni muhimu ukahakikisha unajali sana hali ya akili na mwili wako na kwa kufanya hivyo utatengeneza maisha mazuri unayostahili.
Ulaji vyakula vinavyoishi: Hatua kubwa kupata afya na mwili imara!
Watu wa kale kutoka jamii ya “yogis” huko milima ya “Himalayas” ni watu wanaotoa somo zuri sana juu ya suala zima la kuishi maisha marefu, nishati/nguvu ya mwili na uimara wa mwili na akili.
Wengi wao tunaambiwa ni watu wanaoweza kuishi maisha ya zaidi ya miaka 100 na kudumisha uwembamba na miili imara yenye nguvu sana maisha yao yote, na kuweza kufanya shughuli nzito zinazohitaji ujasiri mkubwa vizuri.
Watu hawa wanaweza kukaa hadi zaidi ya wiki moja bila kula chakula na bila usingizi. Pia, ni watu wenyekuwa na uvumilivu wa kipekee ambao wanaweza kuvumilia maumivu makali sana. Ni siri gani iliyopo juu ya maisha marefu na ya ujana kwa watu hawa? Jibu ni rahisi kwamba, huwa wanajitahidi kula chakula kiasi na wanafuata utaratibu wa kula vyakula vinavyoishi au hai na vya asili.

Kwa taarifa ni kwamba vyakula vinavyoishi ni vile ambavyo vimekuwepo au vimetokana na njia ya asili ambayo ni muunganiko wa nishati ya jua, hewa, udongo na maji. Lishe yenye vyakula vya namna hii, inasisitiza matunda (na juisi zake), mbogamboga na nafaka. Kwa kuweza kufanya mabadiliko na kuhakikisha asilimia 70 ya lishe yako inakuwa ni matunda, mbogamboga na nafaka, utakuwa umepiga hatua ya kwanza kuelekea uimara wa mwili na maisha yenye hamasa kubwa.

Hapa ni baadhi tu ya faida zilizothibitika ambazo utazipata endapo utaanza kutumia vyakula vinavyoishi ni pamoja na kuongezeka kwa kiwango kikubwa cha nguvu zako na stamina; kuongezeka kwa utulivu wa akili na ubunifu; kupungua kwa kitambi na mafuta mwilini; kulainika kwa ngozi; kupungua kwa mahitaji ya usingizi, chakula kusagika kwa urahisi; kuongezeka kwa uchangamfu wa akili; kuwa na kumbukumbu nzuri; maisha marefu na athari kidogo za magonjwa; kuwa na hali ya kujisikia utulivu utokanao na kuwa na hali nzuri kiafya kwa ujumla.

Lishe ambayo imesheheni mbogamboga, nafaka na matunda, ndio hasa asili yetu ililenga kutupatia sisi binadamu. Kwa mfano, meno yetu na utumbo wetu unatofautiana sana na ule wa wanyama wanaokula nyama kama mbwa, LAKINI meno yetu yanafanana na wanyama wanaokula matunda.
Kutoka kwenye nyama kama vile ya ngombe, mbuzi, kuku n.k utupatia lishe ambayo ni ya daraja la pili kwa umuhimu mwilini. Nyama inakuwa kwenye daraja la pili kwasababu inapatikana kwa myama anayekula nyasi, mbogamboga na matunda ya asili.
Kimsingi bidhaa kama nyama imeonekana kuwa na matokeo hasi mwilini na pia inakosa kiasi kikubwa cha vitamini na madini muhimu katika ustawishaji wa mwili wa binadamu. Madini na vitamini ni viasili ambavyo vinahitajika mwilini ili huweze kufanyakazi vizuri na kwa ufanisi mkubwa.
Jambo lingine muhimu kulifahamu ni kwamba, nyama ni chakula kigumu kusagika tumboni, na kwa maana hiyo ni chakula kinachosagwa kwa kuhitaji kiwango kikubwa cha nishati. Matokeo yake, kusagwa kwake kunamaliza kabisa ile nishati/nguvu yote iliyohifadhiwa mwilini na ambayo kama isingepotea kusaga nyama, ingeweza kutumika kufanya kazi nyingine za uzalishaji mali. Ebu jaribu kulinganisha jinsi ujisikiavyo mara baada ya kula nyama steki, na mara baada ya kula mbogamboga na matunda au saladi?
Vyakula vya asili kama vile matunda vinasagika kwa urahisi sana tumboni na vinatumia nishati kidogo sana. Maana yake ni kwamba, ulaji wa vyakula hivi unauachia mwili kiasi kikubwa cha nishati ambayo inakuwepo kwaajili ya kufanya shughuli nyingine muhimu, hasa zile za uzalishaji na shughuli nyinginezo za kutimiza ndoto zako.
Siri mojawapo ya kufanya kazi kwa bidii na bila kuchoka ni uwepo wa hifadhi kubwa ya nishati mwilini. Unaweza ukawa unawahi shambani, ofisini, na mahala pengine, lakini kama huna hifadhi ya nishati ya kutosha mwilini ni kazi bure. Maana utakuwa unachoka haraka kila unapoanza kazi za siku husika.
Kwa wale tunaofanya kazi maofisini ni mashahidi wa sisi wenyewe au marafiki zetu wanaosinzia ofisini na kwenye vikao – tatizo hili linasababishwa na uhaba wa nishati mwilini ambayo kila mara inatumika zaidi kusaga vyakula kama nyama n.k.
Kama nyama ni kitu kibaya kwetu, kwanini tunaila? Watetezi wengi wa ulaji wa nyama wanadai kwamba, ulaji wa mbogamboga hautoi protini inayotakiwa mwilini. Lakini, hiyo tunaweza kusema kuwa ni kejeli kwasababu, wale walao nyama siku zote upata protini isiyokuwa bora kwa binadamu.
Ukweli ni kwamba protini ya kutoka kwenye nyama ina tindikali (acid) hatari mwilini aina ya “Uric acid” ambayo lazima ivunjwevunjwe na ini jambo ambalo linaweza kuleta athari za kiafya siku za mbeleni.
Mbogamboga na matunda pamoja na bidhaa zingine za wanyama kama vile; maziwa ni chanzo cha protini yenye ubora wa hali ya juu (daraja la kwanza) kuliko ile itokanayo na bidhaa za nyama. Ushahidi uliopo ni kwamba unahitaji kuangalia mnyama mwenye nguvu nyingi duniani. Tembo, Faru, Nyani – (wanyama hawa wana nguvu mara 30 zaidi ya binadamu), na wote wanaweza kuishi kwa kutegemea majani, mbogamboga, na matunda. Matunda na mbogamboga vitakupatia protini unayohitaji ambayo ni ya daraja la kwanza.



Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel