Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Ili Uwe Kiongozi Mzuri Kazini.

Kuwa kiongozi bora kazini inatakiwa kujifunza. Kuwa kiongozi kazini huwa haitokei kama ajali bali mtu husika anatakiwa kujifunza namna ambavyo anatakiwa kuwa hivyo. Hivi hujawahi ona umeajiriwa sehemu fulani lakini miaka nenda mika rudi hujawa kuwa kiongozi hapo ofisini hata siku moja? Unafikiri ni wapi ambapo huwa unakosea?
Kama hujawahi kufikiri ni wapi ambapo uwa unakosea basi naomba nikupe mbinu hizi ambazo zitakusaidia kwa namna moja ma nyingine ili uweze kuwa na wewe ni kiongozi siku moja hapo ofisini kwako kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
 Unatakiwa kujifunza kutoa maamuzi.
Miongoni mwa mambo yatakayokusaidia kuwa kiongozi bora katika kampuni ni pamoja na kuwa na uwezo wa kutoa maamuzi, na si maamuzi tu bali na maamuzi mazito yaliyojawa na mtazamano chanya wa kuinuia au kuijenga ofisi yako.
Watu wengi wamekuwa wakichemka sana katika hili, yaani unakuta mtu fulani kafanya kosa fulani kazini ila anashindwa kumuwajibisha mtu huyo, jambo hili ndilo tunaloita kukosa mtazamo na mwongozo wa namna ya kutoa maamusizi sahihi juu ya mtu huyo.
 Uwezo wa kutafuta majibu ya changamoto.
Ili uwe kiongozi bora katika kampuni au ofisi yako basi uanatakiwa kuwa ni kinara wa kutafuta majibu ya kila changamoto inayojitokeza katika kampuni au ofisi uliyopo, kila changamoto inayojitokeza katika ofisi fulani basi haitakiwa kuwa kikwazo cha ofisi hiyo kufanya kazi zake kwa ufasaha bali wewe kama mmoja kati ya wadau wa ofisi hiyo unatakiwa kiongozi na mstari wa mbele katika kutatua  changamoto hiyo kwa kutafuta majibu sahihi.
Uwezo wa kushirikiana na watu wengine.
Unapokuwa unafanya kazi fahamu kuwa ushirikiano na nguvu, na utengano ni udhaifu. Hivyo kila wakati ili uwe kiongozi mwema kazini basi unatakiwa kuelewa namna sahihi inayoweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine kuweza kusaidia katika kutekeleza majukumu ya kiofisi ili kampuni au taasisi iweze kusonga mbele kimafanikio kwa namna moja ma nyingine.
Miongoni mwa faida utakazozipata pindi utakapoamua kuwa na ushirikianao na watu wengine ni kwamba utaweza kujifunza mambo mbalimbali ambayo hapo awali wewe ulikuwa hauyajaui. Pia kufanya kazi kwa ushirikiano husaidia sana kuongeza kasi ya utendaji wa kazi husika, kwa mfano kazi iliyotakiwa kufanywa kwa muda mrefu basi  kazi itafanyika kwa  muda mfupi.
Hivyo kila wakati unatakiwa kubeba dhana hii “kufanya kazi kwa ushirikiano ni chachu ya maendeleo” hivyo hakikisha unakuwa ni mtu wa kushirikiana na watu wengine kadri uwezavyo ili kuweza kuleta maendeleo.
Uwezo mzuri wa kuwasiliana.
Jambo jingine litakalokusaidia kwa namna moja ama nyingine ili kuwa kiongozi mzuri  wa kiutendaji katika kazi yako ni vile ambavyo utaamua na kulibeba jukumu la kuweza kuwasilina vyema na watu wengine.
Namna ambavyo utaweza kuwasiliana vyema na wafanyakazi wengine, namna ambavyo utakuwa una uwezo wa kuongea na wateja ndivyo ambavyo watu watakavyozidi kukuamini au kuiamini ofisi ambayo unaifanyia kazi.
Ukiweka kinyongo na maslai mengine binafsi nyuma husasani suala la mawasiliano ndivyo ambavyo utavyokuwa unaiua kampuni pasipo wewe mwenyewe kujua.
Mtu mmoja aliwahi kusema “watu mara nyingi huwa hanunui bidhaa yako tu, bali hununua mahusiano yaliyopo kati yake na yako”. Mahusiano haya mara nyingi hujengwa na mawasiliano yaliyo kati yako na yake. Hivyo kila wakati ili uweze kuwa ni mmoja kati ya watu wenye chachu na shauku kubwa ya kufanya vizuri katika jambo unalolifanya basi unatakiwa kuwa ni mtu ambaye unadumisha mawasilaino yenu yaliyopo kati yako na wateja wako.
Ndimi Afisa Mipango: Benson Chonya
0757-909942

Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel