Jinsi Umaskini Unavyomaliza Maisha Yako.

Na Eryne Banda, Dar es salaam.
Umaskini ni kutokuweza kumiliki kitu chochote katika maisha iwe ni nyumba, gari, shamba, ardhi na kadhalika. Ni kuishi kwa kusaidiwa na watu. Hapa mtu anakuwa hana uwezo wa kujisimamia, anaishi kwa kuombaomba.
Nikumbushe kwamba umaskini umechangia tribu nyingi kutikisika kiuchumi, zingine zikisambaratika kabisa. Umaskini umesababisha afya mbaya katika baadhi ya tribu huku wengine wakishindwa kuwapa elimu bora watoto wao.
Pamoja na hayo kabla hatujaingia kwenye somo jinsi umaskini unavyoweza kukumaliza, naomba tuangalie kwanza, aina mbalimbali za umaskini ambazo zimetuzunguka na zinaendelea kutesa wengi pasipo kujua chanzo chake.

Umaskini wa mawazo.
Huu ni umasikini mbaya sana. Watu wengi wana fedha lakini hawana mawazo mapya. Umaskini wa mawazo ni mbaya kuliko umaskini wa mali. Jamaa mmoja aliwahi kusema “mwisho wa mawazo yako ndio mwanzo wa matatizo yako”. Tatizo la matajiri wengi ni kutokuwa na mawazo mapya japokuwa wana fedha nyingi.
Yapo mapepo yaliyofunga akili za watu ili wasiwe na mawazo mapya. Mawazo mapya yanatoka kwa Mungu, hivyo tunapaswa kumuomba Mungu kwa bidii ili atupe mawazo mapya. Je, jiulize hapo ulipo upo tayari kujenga mawazo mapya kwa kiasi gani au bado unataka kuendelea na mawazo yako yaleyale?
Umaskini wa tabia.
Mtu mmoja aliwahi kusema; karama itakupeleka juu lakini tabia itakufanya uendelee kubaki chini. Watu wengi wana karama nzuri, vipawa vizuri lakini wameshindwa kwenye tabia. Watu wengi wamefukuzwa kazi kwa sababu ya tabia zao mbaya huku wengine wakipewa majina mabaya sababu ya tabia zao.
Ni vema sote tukaelewa kwamba; tabia yako ndiyo inayokutambulisha kwa watu; ndiyo itakayokupa kibali; ni wakati upo peke yako; yale mambo unayoyafanya wakati wengine hawakuoni. Tabia yako ndiyo itakayokufanya uendelee kuwa maskini au uwe tajiri; ndiyo inayokufanya udharauliwe au uheshimiwe.
Ni muhimu sana kumuomba Mungu abadilishe tabia yako ili iwe nzuri na ndipo utakapofanikiwa. Usiposhughulikia tabia yako, tabia itakushughulikia wewe. Watu wengi watakupenda kwa sababu ya tabia yako nzuri. Kumbuka: Utajiri wa tabia ni zaidi ya utajiri wa fedha/mali. Maisha ndivyo Yalivyo.
Umaskini wa marafiki.
Mafanikio yanahitaji uwe na watu wazuri na hakika, huwezi kufanikiwa peke yako. Watu wengi wamekosa kuwa na marafiki wazuri ndiyo maana wameshindwa kufanikiwa. Umaskini wa marafiki ni kuunganishwa na marafiki wabaya ambao ni chanzo cha kuangamiza hatma yako.
Kwa mfano, ili Daudi respeto mfalme, Mungu alimuunganisha na Yonathani ili aje kuwa mfalme. Bila ya Yonathani, Daudi asingekuwa mfalme hata kama alikuwa amepakwa mafuta.
Alihitaji mtu wa kumshika mkono na kumfikisha kwenye kiti chake cha ufalme. Soma andiko la Mungu katika 1Samweli 18: 3, “Nao Yonathani na Daudi wakaahidiana, kwa kuwa alimpenda kama roho yake mwenyewe.”
Mpenzi msomaji, wapo watu ambao Mungu amewaandaa ili waweze kukufikisha kwenye hatma yako. Mungu anaweza kukuunganisha na mtu mmoja tu na maisha yako yakabadilika.
Tazama marafiki zako ulio nao, ndipo unapoweza kufanikiwa kwani huwezi kufanikiwa peke yako. Ni lazima uwe na watu wazuri wa kukusaidia. Muombe Mungu akuunganishe na marafiki wazuri, watu wenye bidii kuliko wewe.
Naamini msomaji wangu umejifunza jambo hapo. Tuishie hapa hadi wiki ijayo ambapo nitaendeleza kidogo mada hii muhimu kwa kutaja aina zaidi za umaskini ili uweze kujijua kinachokusibu hapo ulipo.
Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kwa ajili ya kujifunza na kumasika kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Makala hii imeandikwa na Eryne Banda wa Dar es salaam, Tanzania.

Iklan Atas Artikel

Iklan Tengah Artikel 1

Iklan Tengah Artikel 2

Iklan Bawah Artikel